Mahakama ya Mbulu yamhukumu Mama kwa Kumficha Mwanae Anayetuhumiwa Kulawiti - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 28 August 2024

Mahakama ya Mbulu yamhukumu Mama kwa Kumficha Mwanae Anayetuhumiwa Kulawiti




 Na Epifania Magingo,Babati 


maipacarusha20@gmail.com 


Hatimae Mahakama ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara imemuhukumu Anna Burra Mkazi wa kijiji Cha Moringe Kata ya Daudi kutumikia kifungo Cha miezi sita Gerezani, baada ya kushindwa kumleta Mshtakiwa Carol Christopher ( 18)anaekabiliwa na kosa la kumlawaiti mtoto mwenye umri wa miaka miwili na miezi tisa aliyekuwa amemdhamini katika kipindi chote Cha mwenendo wa shauri hilo.


Anna Burra, Mama mzazi wa Carol kabla ya kuhukumiwa kifungo hicho Agosti 21 mwaka huu,siku ambayo ilikua rasmi kwa Mahakama hiyo kutoa hukumu kulingana na mwenendo mzima wa shtaka hilo kama Mdhamini aliambia Mahakama hiyo kuwa Mshtakiwa Carol hakuweza kufika Kutokana na kusumbuliwa na tumbo la kuhara na kulazimika kwenda Mkoa Arusha kupata matibabu kwenye hospital ya Seliani.


Hata hivyo, Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mwendesha Mashtaka Mkaguzi wa Polisi Maraba Masheku uliridhia Ombi hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mheshimiwa Johari Kijuwile ukimuamuru kufika na Mshtakiwa Carol pamoja na vielelezo vinavothibitisha kulazwa seliani Jijini Arusha lakini alishindwa kutekeleza.


Mbele ya meza ya hukumu baada ya Anna Burra aliyefika na mtoto mgongoni tofauti na siku nyingine alipotakiwa na Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Mkaguzi wa Polisi Maraba Masheku uliokua tayari kusikiliza hukumu lakini Mdhamini huyo aliambia Mahakama kuwa Mshtakiwa Carol hapatikani kwa njia ya simu na hajui kwanini hapatikani.


Aidha,akiiomba Mahakama hiyo Mkaguzi Mahakama kutoa hukumu kufuatia Mdhamini kuonekana kuidanganya Mahakama huku pia alishindwa kuwasilisha vielelezo alivyotakiwa, Masheku aliomba Upande wa Mshtakiwa kuwasilisha dhamana ya msharti shillingi milioni tatu lakini pia kupitia kifungu Cha 160(4) sura ya 20 ya  mwaka 2022 Upande wa Jamhuri kuridhia ombi hilo sambamba na kifungo Cha miezi sita kwa Anna Burra.


Kufuatia ombi la Jamhuri ndipo Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi Mheshimiwa Johari Kijuwile aliporidhia kutoa adhabu ya kifungo hicho kufuatia Mshtakiwa kuruka dhamana lakini pia kuwasilisha fungu la ahadi ya dhamana la kiasi Cha shillingi milioni tatu ambazo alishindwa kulipa.


Hata hivyo Hakimu Kijowile ameamuru Mahakama kuota hati ya kukamwatwa kwa Carol Christopher kabla ya Mahakama hiyo kutoa hukumu Agosti 28,2024.

No comments: