Meya Tanga awavutia wawekezaji wa biashara - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday 29 August 2024

Meya Tanga awavutia wawekezaji wa biashara

Meya wa jiji la Tanga,Abdurahman Shiloo akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la ving'amuzi vya Azam jijini Tanga.Picha na Burhani Yakub

Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Shehoza, Latifah Makau Shehoza akizungumza wakati wa uzinduzi wa duka la ving'amuzi vya Azam jijini Tanga





Na: Burhani Yakub,Tanga


maipacarusha20@gmail.com 


Sekta binafsi imehimizwa kuongeza kasi ya kuweka miradi katika jiji la Tanga ili kuongeza pato la wananchi kupitia ajira pamoja na kuzidisha pato la Taifa kupitia vivutio mbalimbali ikiwamo historia na utamaduni uliopo.

Wito huo umetolewa na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Abdurahman Shiloo alipokuwa akizindua duka la kuuza ving’amuzi vya Azam mjini hapa.

Alisema kwa kuwa Tanga ni mji wenye historia, utamaduni na fursa nyingi ikiwamo ukarimu wa watu wake unaoujulikana hadi nje ya mipaka ya nchi, sekta binafsi inapaswa kuchangamkia fursa hiyo ili kuwaletea ajira wakazi wake.

“Tumeanaza kuona mabadiliko chanya yanayoletwa na uwekezaji ndiyo maana Halmashauri ya Jiji inaunga mkono kampuni mbalimbali binafsi ikiwamo Azam kupitia ving’amuzi vyake”amesema Shiloo.

Amesema huduma hiyo itaondoa usumbufu walioukuwa wakiupata wananchi kusafiri hadi jijini Dar es salaam kufuata bidhaa zitokanazo na ving’amuzi hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Shehoza ambayo ndiye wakala wa ving’amuzi vya Azam, Latifah Makau amesema lengo la kufungua duka hilo ni kuwawekea karibu wakazi wa Tanga huduma ya ununuzi wa ving’amuzi na bidhaa nyingine za Azam badala ya kuzifuata mbali.

“Kupitia Azam wakazi wa Tanga wataweza kufuatilia vipindi vya maana vyenye uadilifu na maadili mema bila kuwasahau wapenzi wa michezo ambao sasa wanaweza kufurahia mechi za soka si tu vilabu vya Simba ,Yanga,Azam FC bali pia timu yetu pendwa ya Coastal union”amesema Latifah.

MWISHO.

No comments: