MNADA WA MBAAZI WA KIELEKTRONIKI WAZINDULIWA MVOMERO DC MVOMERO AAHIDI KULA SAHANI MOJA NA WANAOCHEPUSHA MAPATO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 28 August 2024

MNADA WA MBAAZI WA KIELEKTRONIKI WAZINDULIWA MVOMERO DC MVOMERO AAHIDI KULA SAHANI MOJA NA WANAOCHEPUSHA MAPATO

 






MKUU wa Wilaya ya Mvomero Judith Nguli



Na Lilian Kasenene, Morogoro

maipacarusha20@gmail.com 


Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judith Nguli amesema ataendelea kuwachukulia hatua wafanyabiashara wanao kwepa kulipa kodi kutokana na kutofuata taratibu wakati wa kununua mazao kutoka kwa wakulima ikiwemo matumizi ya mfumo wa stakabadhi ghalani.


Nguli alitoa kauli hiyo wakati akizindua Mnada wa kwanza wa Mbaazi kwa mfumo wa Stakabadhi Ghalani uliofanyika kwenye ghala lililopo katika Kata ya Sungaji, Kijiji cha Mbogo.


Mkuu huyo wa Wilaya alibainisha kuwa Halmashauri hiyo kupitia Baraza la Madiwani liliazimia mazao ya Ufuta, Alizeti, Mbaazi na Korosho yauzwe kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani lengo ni kuwainua wakulima ambao wanatumia gharama kubwa kwenye kilimo wakitarajia kupata faida.


“Na mimi nitaendelea kuyakamata magari yanayo torosha mbaazi, tena nitayakamata pasipo huruma," alisema Mkuu wa Wilaya.


Aidha, alisema Serikali inatekeleza maelekezo ya Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ibara ya 34 ambapo imeelekeza mazao yote ya kimkakati yaingizwe kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani ili kumuinua mkulima.


Naye Afisa Kilimo wa Kata ya Sungaji Clemence Kakuo amesema mfumo huo unalenga kuwaondoa walanguzi ambao wamekuwa wakinufaika kwa kununua mazao ya wakulima kwa shillingi 30,000 kwa debe huku wao wakiuza kwa bei ya juu hivyo amesema kupitia mnada huo mkulima anatarajia kupata shillingi 40,000 kwa debe.


Aliongeza kuwa hadi kufikia Agosti 27, 2024 jumla ya tani 95 ambazo zinatarajiwa kuuzwa kwa njia ya kielektroniki ambapo wanunuzi na bei ya mazao yatafanyika kwa njia ya mtandao.


Mwisho.

No comments: