RAIS SAMIA AVITAKA VYUO VIKUU KUFANYA TAFITI ZITAKAZOSAIDIA TAIFA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 6 August 2024

RAIS SAMIA AVITAKA VYUO VIKUU KUFANYA TAFITI ZITAKAZOSAIDIA TAIFA

 






Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amevitaka vyuo vikuu nchini kuweka nguvu ya pamoja katika kufanya tafiti mbalimbali zinakazosaidia jamii na Taifa katika magonjwa mbalimbali.


Pia amevitaka vyuo vinavyojihusisha na tafiti mbalimbali kuhakikisha tafiti hizo zinawafikia walengwa na kufanyiwa kazi badala ya kuishia katika mashindano ya tuzo za Maprofesa.


Rais Samia alisema hayo wakati akizindua Jengo Mtambuka la Mafunzo Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo(SUA) kilichopo mkoani Morogoro,ambapo jengo hilo limepewa jina la Samia Suluhu Hasaan Teaching Complex lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 3,205 kwa wakati mmoja.


Aliseama Serikali ilitoa kiasi cha shilingi bilioni 9 ambapo bilioni 2.6 ili kukamilisha ujenzi  huo wa jengo lenye viwango vya kimataifa ambalo litatumika kwa wanafunzi wa ndani ya nchi na nje.


" Nimefurahi mmejiongeza, serikali imewapa fedha nanyi mkajiongeza, unaambiwa ukifiwa wanapokuja watu kuzika na wewe lazima ubebe jeneza,"alisema.


Rais Samia alisema jengo hilo litatumika katika tafiti mbalimbali na kuwataka tafiti hizo wasibaki nazo na badala yake ziwafikiwe walengwa ili kuleta matokea ya tafiti hizo.


Alisema tafiti hizo zimesaidia kutoa matokea ya mbegu nzuri mfano za migomba na kwamba zikitumika vizuri zitasaidia bidhaa za Tanzania kuuzwa nje bila vikwazo vyovyote kwani zitakuwa na ubora wa kimataifa.


Aidha Rais Samia alisema kukamilika kwa jengo hilo kumewezesha wanafunzi kutoka mataifa ya nje ya nchi kuja kusoma hapa nchini tofauti na ilivyozoeleka awali Watanzania ndio walikuwa wanaenda nje kusoma.


Alisisitiza matumizi mazuri ya fedha zinazotolewa na wafadhili ili waweze kuendelea kutoa fedha hizo kwaajili ya miradi mbalimbali hapa nchini


Pia aliwataka kuhakikisha jengo hilo linatunzwa na kuendelea kubaki katika ubora wake na viwango vilivyopitishwa Kimataifa.


Alisema matumaini yake kuona wanafunzi wanamaliza chuoni hapo wanaingia katika sekta mbalimbali za kilimo ili kutumia ujuzi wao kuleta tija kwa taifa.


Awali  mkuu wa Chuo  Kikuu cha Sokoine  cha kilimo Sua Jaji  mkuu mstaafu Joseph Sinde Warioba alisema asilimia 92 za Tafiti zinazofaanywa SUA zinafadhiliwa na mataifa ya nchi na kwamba tafiti hizo ni zile zenye tija kwao na kwamba asilimia 8 tu ndio zinafadhiliwa ndani ya nchi.


Alisema Serikali inaendelea kuangalia uwezekano wa kuwezesha tafiti mbambali zenye tija hapa nchini ili kutanua wigo mkubwa wa tafiti hapa nchini.


Kwa  upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Adolf Mkenda alisema serikali imekuwa ikitoa tuzo kwa watafiti mbalimbali kiasi cha shilingi milioni 50 kwa mtafiti anayechapisha tafiti zake zinazohusu masuala ya Sayansi, elimu tiba na tehama.


Alisema lengo ni kuhakikisha tafiti hizo zinaonekana kimataifa badala ya kuishia hapa nchini.


Hata hivyo alisema  zipo tafiti mbalimbali zenye matokeo chanya ikiwemo ya chanjo ya  kuku ya ugonjwa wa mdondo au Kideri inayoweza kutumika katika kukinga mifugo .


Alisema tafiti nyingine imegundua mbegu bora ya maharage inayohimili ukame na magonjwa mbalimbali .


Pia alisema ipo miche ya matunda mbalimbali ambayo inaweza kutumika katika maeneo mbalimbali.


Mwisho.

No comments: