Wakili Mwabukusi Ashinda Urais wa TLS - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 2 August 2024

Wakili Mwabukusi Ashinda Urais wa TLS

Wakili Boniface Mwabukusi aliyeshinda nafasi ya Urais wa TLS 


Na Mwandishi Wetu, maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


WANACHAMA wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) wamefanya Uchaguzi wa Haki kwa kumchagua wakili msomi na maarufu nchini Boniface Mwabukusi kuwa rais wa chama hicho.


Mwabukusi ametangazwa mshindi wa kiti hicho kwa kupata kura 1,274 ambazo ni sawa na asilimia 63.1 dhidi ya washindani wake Sweetbert Nkuba, Revocutus Kuuli, Ibrahim Bendera, Paul Kaunda na Emmanuel Muga katika uchaguzi ambao kwa mara ya kwanza umefanyika nje ya Jiji la Arusha.


Kinyang'anyiro cha uchaguzi huo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC) jijini Dodoma, kililenga kumpata mrithi wa Harold Sungusia aliyemaliza muda wake.


Matokeo ya uchaguzi huo yalitarajiwa kutangazwa saa 11 jioni, lakini yametangazwa saa 5. 15 usiku huu.


Matokeo yamechelewa kutangazwa tofauti na ilivyotarajiwa, kutokana na msiba wa mmoja wa wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho, Maria Pengo na kusogezwa muda kutokana na karatasi za kura kupungua.

No comments: