AUWAWA KWA KUCHOMWA KISU KISA SH 200 YA KAMARI YA POOL TABLE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 30 September 2024

AUWAWA KWA KUCHOMWA KISU KISA SH 200 YA KAMARI YA POOL TABLE

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Alex Mkama


Na Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


MTU mmoja Hussein Nyabu Steven(35) dereva na mkazi wa Ngerengere Kaskazini ameuwawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani baada ya ubishani wa shilingi mia mbili(200) na mwenzake wakati wa mchezo wa kamari ya Pool Table.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Alex Mkama alisema hayo wakati wakitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya tukio hilo la mauaji lililotokea Septemba 29,2024 saa moja usiku.


Mkama alisema kutokana na tukio hilo mtu mmoja Kulwa Bosco(27) maarufu kama Rasta,mfugaji na mkazi wa kijiji cha Sinyaulime tarafa ya Ngerengere wilaya ya Morogoro anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma za mauaji hayo.


Alisema marehemu pamoja na mtuhumiwa walikuwa katika mchezo wa kamariya pool table baada ya kubishania shilingi mi mbili ndipo mtuhumiwa alitoa kisu na kumchoma marehemu.


Jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linatoan wito kwa wananchi hususani vijana kuacha kujichukulia sheria mkononi, huku likiwataka kujikita kwenye kufanya kazi ili kujiingizia kipato cha halali na si kutegemea kamari.


Mwisho.

No comments: