DC Hanang' AWATAKA Wananchi kuwapigia kura Viongozi waadilifu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 30 September 2024

DC Hanang' AWATAKA Wananchi kuwapigia kura Viongozi waadilifu






Na Epifania Magingo, Babati 


maipacarusha20@gmail.com 


Kuelekea Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za mitaa ambao utakaofanyika 27 Novemba 2024,Mkuu wa Wilaya ya  Hanang' Mkoani Manyara Almish Hazali àmetoa rai kwa wananchi kujitokeza kwa wingi na kushiriki kikamilifu  kupiga kura ili kupata kiongozi bora na mwenye nia ya maendeleo.


Akizungumza mara baada ya ibada ya Uzinduzi wa Kanisa la Elim Pentekoste Tanzania,Kata ya Jorodom Wilaya ya Hanang, kiongozi huyo amesema ni  kila mwananchi anahaki ya kumchagua  kiongozi ambae anaona ana uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii na Taifa kwa ujumla.


Aidha, Almish amewatoa hofu wakazi wa Wilaya ya Hanang'  na kusema  kuwa uchaguzi huo utafanyika  kwa amani na utulivu kwakuwa ulinzi na usalamà umezidi kuimarishwa katika wilaya ya hiyo.


"Wilaya yetu ya Hanang,Ipo Shwari  naomba wananchi wote wa Hanang Tuwe na Amani  Maeneo Yote,maneno mnayosikia ni Maneno ya mtaani lakini Serikali muda wote ipo na ninyi wananchi wake"Amesema Almish 


"Tumeona taarifa kwenye vyombo vya habari watoto wanapotea kwa mazingira ya utatanishi, kwa kweli hatuna amani ila kwa sababu mkuu wa wilaya ametuambia kuwa kuna ulinzi, tunaomba uendele  uimarishwe  hasa maeneo yetu hayà ya vijijini"Alisema Selina Sixtbet Mkazi wa wilaya Ya Hanang


Kwa Upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Elim  Pentekoste Tanzania Askofu Peter Konki akizungumza wakati wa kuweka wakfu Jengo la  Kanisa la Elim Pentekoste Jorodom amewatahadharisha wananchi  kuwa makini dhidi ya viongozi wanaowarubuni kwa zawadi ili waweze kuingia madarakani.


"Kuuza Kura ni  Kujinyima haki ya msingi,Kila mmoja aende apige kura  na kumchagua kuongozi sahihi,kura ni Maamuzi kuuza kura ni kijinyima maamuzi na kuweka kichwa chako kwenye mfuko wa mwenye Elfu Tano, Jambo hili Halikubaliki"Amesema konki


Hata hivyo baadhi ya wananchi wamekiri kujawa na hofu Kutokana na uwepo wa taarifa za hivi karibuni za matukio ya watoto,kuuwawa na kutolewa Figo.

No comments: