DCEA YASHIRIKI KIKAO CHA MWAKA CHA MAAFISA USTAWI WA JAMII MKOANI KILIMANJARO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday 20 September 2024

DCEA YASHIRIKI KIKAO CHA MWAKA CHA MAAFISA USTAWI WA JAMII MKOANI KILIMANJARO

 


Na Prisca Libaga Kilimanjaro


maipacarusha20@gmail.com 


Ofisi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imeshiriki Kikao cha Mwaka cha Maafisa Ustawi wa Jamii kuanzia tarehe 18 hadi 20 Septemba 2024 kilichofanyika Ukumbi wa CCP Moshi mkoani Kilimanjaro.


Lengo la Kikao hiko ni kuwakutanisha Maafisa Ustawi wote nchini kujadili afua mbalimbali za kuwasaidia watu waliopo kwenye Makundi Maalum kamavile kundi la waraibu wa dawa za kulevya. Kauli mbiu ya mwaka huu ni _"Tanzania bila Ukatili Inawezekana, Imarisha Mahusiano Chanya ya Familia"_.


Kikao kilifunguliwa na Naibu wa Waziri wa Fedha Mh Hamad Chande na Kufungwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt Doroth Gwajima ambaye katika hotuba yake amewahakikishia Maafisa Ustawi wa Jamii kuwa na Idara yao ambayo itakuwa inajitegemea. 


Aidha amewapongeza Maafisa Ustawi Jamii wa kuendelea kujitoa zaidi katika utekelezaji wa majukumu yao. 


Mwisho.

No comments: