Hanang' Walia na Mwenyekiti RUWASA awapatie maji safi na salama - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 24 September 2024

Hanang' Walia na Mwenyekiti RUWASA awapatie maji safi na salama

 




Na, Epifania Magingo, Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Wananchi wa Wilaya ya Hanang' Mkoani Manyara ambao hawajafikiwa na huduma ya maji safi na salama wameiomba Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kuongeza visima vya maji safi ili kuondokana na matumizi  ya maji ya visima kutoka kwenye makorongo ambayo sio salama kiafya.


Wakizungumza mbele ya Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA Taifa Ruth Kayo katika ziara yake ya  ukaguzi wa utekelezaji wa mpango wa uchimbaji wa visima 900 Nchini katika vijiji vya Gisambala pamoja na Kinyamburi  Wilayani Hanang' wananchi hao wemesema kuwa shida hiyo imekuwa ikiwalazimu kutembea umbali mrefu kufuata  huduma ya Maji safi na kuomba kuongezewa miundombinu ya visima vya maji  yatakayo saidia kutatua changamoto hiyo kwa vitongoji ambavyo havina huduma ya maji safi.


"Bado Serikali tunawahitaji sana,Bado hitaji letu liko pale pale kwasababu Kijiji Cha Kinyamburi ni kikubwa sana tumepakana na vijiji 2 kijografia Wananchi wengine wako mbali na kisima hiki, tunamshukuru tumepata kisima hiki lakini uhitaji wetu maji yatawanywe yawafikie na wengine"Simoni Akonaay amesema


"Tunashuru kwasababu tulikua tunapata maji hadi uchimbe mchanga, Chini ya mchanga ndio tulikua tunapata maji, lakini mradi huu utatusaidia huku Kijiji Cha gisambala pia  watoto wetu watapata maji na wataoga vizuri kama watoto wengine" Helena Bombo amesema


Meneja wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA )Wilaya ya Hanang' Herbet Kijazi amesema  Bado serikali inaendelea kuchimba visima ili kuhakikisha kila mwananchi anafikiwa na huduma ya Maji safi na salama.


"Mradi huu unalengo la kuwahudumia Wananchi wengi wenye uhitaji wa maji na itasaidia kupunguza adha ya Wananchi kufata maji kwa umbali mrefu".Kijazi amesema 


Mwenyekiti wa Bodi ya  RUWASA Taifa Ruth Kayo amesema  Mpango wa Uchimbaji Visima 900 nchini unalenga kujenga visima 5 kwa kila Jimbo ambapo kilà mwananchi atapata Huduma ya maji safi na salama.


"Mheshimiwa Rais amesema Kila Kijiji ambacho hakina maji kiwekewe miundombinu ya maji,na mpaka kufikia December 2024 Kila Kijiji kiwe kimepata maji". Ruth amesema


Imeelezwa kuwa  mradi huo umegarimu milioni 25 ukiwa na lengo wa kuwahudumia Wananchi wengi wenye uhitaji wa maji na kupunguza adha ya Wananchi hao kutafuta maji kwa umbali mrefu usiopungua kilomita 4.

No comments: