Injinia Koya Aridhishwa na Ujenzi wa miradi ya Maji Mbulu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 25 September 2024

Injinia Koya Aridhishwa na Ujenzi wa miradi ya Maji Mbulu

 




Na: Epifania Magingo, Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Mwenyekiti wa Bodi Idara ya Maji Taifa ( RUWASA) Injinia Ruth Koya amekagua miradi ya Maji inayoendelea kutekelezwa kwenye Wilaya ya Mbulu Mji na Vijijini Mkoani Manyara ukiwemo mradi mkubwa wa maji Dambiya Hydom ambao utakwenda kutatua changamoto kubwa ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu ambao utanufaisha Vijiji 21.


Mradi huo ambao ulianza mwaka 2023 unatarajiwa kukamilika 2025 umegarimu zaidi ya Shilingi Billion 41 na unategemea vyanzo 3 vya maji venye visima virefu ambavyo vinauwezo wa kuzalisha kwa pamoja Lita laki mbili na ishirini kwa saa.


Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Injinia Onesmo Mwakasege  amesema mradi huo unatekelezwa kwa vyanzo vitatu vya fedha ikiwemo Serikali kuu utakuwa na manufaa makubwa kwa wananchi zaidi ya laki Moja huku akitaja changamoto za utekelezaji wa mradi huo ni kwamba wanakabiliwa na upatikanaji wa fedha za kumlipa mkandarasi pamoja na kununua pampu Tano.


" Tunamshukuru Rais Samia kwa kuridhia kujengwa  na kutoa fedha za ujenzi,ruwasa makao makuu ,mkuu wa Wilaya na wananchi kwa ujumla kwa kutoa ushirikiano kwa ruwasa ili waweze kushughulikia na kutoa huduma ya Maji kwa wananchi "Mwakasege amesema 


Naye,Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mji Veronica Kessy ametoa ombi kwa Mwenyekiti wa Bodi RUWASA Taifa Ruth Koya kushughulikia upatikanaji wa fedha za miradi hiyo kwa haraka ili iweze kukamilika kwa wakati na wananchi waweze kupata huduma ya Maji.


Mkurugenzi wa RUWASA Taifa,Ruth Koya amesema kama Serikali changamoto zilizotajwa zimepokelewa na zitashughulikiwa kwa jinsi inavotakiwa na kusema kuwa panapotokea changamoto ziwasilishwe mapema ili mradi uweze kumalizika kwa Muda uliopangwa.


"Niwapongeze kwa kazi kubwa mnayoifanya ,tuendelee kushirikiana ili kufanikisha gurudumu la manendelo,na kama Serikali iko tayari kutekeleza miradi,Mheshimiwa Rais amezamiria kumtua mama ndoo kichwani,na sio kwa maneno bali anafanya kwa vitendo".


Baadhi ya Wananchi waliohudhuria wakati wa ukaguzi wa miradi hiyo akiwemo Diwani wa Kata Bashay Calist Calist amesema mradi huo utahudumia wananchi wengi wakiwemo jamii ya Wahadzabe ambao wamekua tatizo la kukosa maji kwa Muda mrefu huku Petro Gishii amesema kwasasa wanatarajia kupata maji kwa wingi hata katika maneno ya miinuko.


Ili kukamilisha utekelezaji wa mradi huo kwa wakati Serikali iliahidi kutoa Gari mbili katika mradi wa Maji Dambiya Hydom  ambapo wakati wa ukaguzi huo ilitolewa gari Moja yenye thamani ya zaid milioni 200.

No comments: