JUKWAA LA JAMII MSIMU WA NNE MOROGORO LAZUNGUMZIA MIGOGORO YA ARDHI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 30 September 2024

JUKWAA LA JAMII MSIMU WA NNE MOROGORO LAZUNGUMZIA MIGOGORO YA ARDHI

 







Na Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


JUKWAA la Jamii mkoa wa Morogoro limeeleza kuwa migogoro mingi ya ardhi iliyopo ndani ya mkoa huo  inasababishwa na baadhi ya watu kununua maeneo bila kujiridhisha vya kutosha ambapo limeshauri wanajamii kutumia wanasheria wakati wa manunuzi kwa eneo la ardhi husika.


Mwanasheria wa Kituo cha Msaada wa kisheria Morogoro(MPLC) Maurine Binyoni alisema hayo wakati wa Kongamano la Jukwaa la Jamii Msimu wa nne lililofanyika mkoni Hapa.


Binyoni alisema ili mkoa wa Morogoro uweze kuondokna na migogoro mingi  ya ardhi iliyopo na inayoendelea kujitokeza mara kwa mara ni vyema wanunuzi wa maeneo mbalimbali kabla ya kununua kujiridhisha vya kutosha ili kuepukana na mgogoro wowote.


“Sasa ningependa kuwashauri ndugu wanajamii ili kuondokana na migogoro ya ardhi na kabla hujanunua eneo kwanza nenda kahakikishe nenda kwenye eneo husikaa je yule anaekuuzia ndiye anayepaswa kukuuzia lile eneo, na mipaka ikoje na majirani wanasemaje, na hiyo itasaidia kufahamu kma kuna migogoro ama la lazima utambue hilo,”alisema.


Aidha alisema kabla ya kununua eneo husika kutumia wanasheria ili kukupa elimu na pindi unafanya mauziano awepo mwanasheria ambaye ataandika hati ya mauziano na kinachotakiwa ni kufika ofisi ya ardhi ndani ya halmashauri husika ili kuangalia hati miliki kama inamuhusu muuzaji.


Aidha Mwanasheria huyo alisema hiyo itasaidia kuondokana na changamoto za migogoro ya ardhi, lazima njia za kuepukana nazo ziangaliwe wanajamii wanatakiwa kutokubali kuuziwa eneo bila kuwa na mkataba.


Mkurugenzi wa MPLC Amani Mwaipaja akizungumzza katika Jukwaa hilo alisema jukwaa hilo lipo kihalisia zaidi nia ni kuwafundisha wanajukwaa kujifunza, kufanya na kufundisha wengine.


“Tunategemea Jukwaa hili kuwafundisha watu kupata fursa zilizopo, tumekuwa tukifanya mikutano kama hii kwenye wilaya tatu za mkoa wa Morogoro ikiwemo Malinyi ambapo tumefanya mikutano kwenye vijiji 12,”alisema.


Mwenyekti wa jukwaa la wanawake kata ya Kihonda Magorofani Mariam Kifyoga alizungumzia suala la ukatili wa kijinsia kwa watoto na wanawake ambapo aliwataka wazazi kuacha tabia ya kukaribisha ndugu zao na kulala na watoto jambo linalofanya watoto hao kufanyiwa ukatili.


“Kizazi chetu kinaangamia, wazazi tuache tabia ya kuaminiana hata ndugu kwa ndugu ,”alisema.


Kauli mbiu ya Jukwaa hilo ni ‘Kujumuika, Kujifunza na Kupeana Fursa’.


Mwisho.

No comments: