KIMESO ACHAGULIWA TENA KUWA MAKAMU MWENYEKITI SIMANJIRO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 3 September 2024

KIMESO ACHAGULIWA TENA KUWA MAKAMU MWENYEKITI SIMANJIRO

 




Na Mwandishi wetu, Simanjiro 


maipacarusha20@gmail.com 


DIWANI wa Kata ya Edonyongijape Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Jacob Kimeso amechaguliwa kwa kipindi kingine cha tatu kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.


Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri huchaguliwa kila mwanzo wa mwaka wa fedha unapoanza na huu utakuwa mwaka wa tatu mfululizo Kimeso ameshika nafasi hiyo.


Awali, Kaimu DED Simanjiro Dominica Ngaleka akizungumza kwenye kikao cha Baraza hilo amesema amepokea barua kutoka CCM inayomtambulisha Kimeso kuwa mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti kupitia chama hicho.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Baraka Kanunga Laizer amesema madiwani wote 25 wamemchagua Kimosa kuendelea na nafasi hiyo.


Hata hivyo, Kanunga amesema wajumbe wa kamati ya huduma za jamii wamemchagua Diwani wa Kata ya Ngorika Albert Msole kuwa Mwenyekiti wao.


Amesema wajumbe wa kamati ya Uchumi, Uenzi, na Mazingira, wamemchagua Diwani wa Kata ya Oljoro Namba 5, Loishiye Lesakwi kuwa Mwenyekiti wao.


Amewataja wajumbe wa ALAT Mkoa ni Diwani wa Kata ya Ruvu Remit Yohana Maitei (Kadogoo) na Diwani wa viti maalum Tarafa ya Naberera, Bahati Mosses Patson na mjumbe kamati ya ajira ni Diwani wa Kata ya Terrat, Jackson Ole Materi.


Akizungumza baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo kwa mara nyingine Kimeso amewashukuru Madiwani hao kwa imani kubwa waliondelea kuwa nayo kwake.


"Tuendelee kushirikiana katika kuhakikisha tunajenga Simanjiro yetu nzuri yenye neema tele na endapo kuna mapungufu au nimewakosea mnisamehe," amesema Kimeso.


Amewaahidi madiwani hao kuendelea kuwapa ushirikiano katika kuhudumu nafasi hiyo ya kumsaidia majukumu Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo.


MWISHO

No comments: