Timu 35 Kupambana Chem Chem CUP 2024,millioni 78 kutumika - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 8 September 2024

Timu 35 Kupambana Chem Chem CUP 2024,millioni 78 kutumika

 










Na: Mussa Juma, maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Babati.Jumla ya timu 35 zinatarajiwa kushiriki michuano ya Chem chem CUP mwaka 2024 ambayo inatarajia kutumia takriban Shilingi 78 millioni.


Michuano hiyo ya 10 kufanyika imezinduliwa Jana  na Mkuu wa mkoa Manyara, Queen Sendiga ambaye aliwakilishwa na Mkuu wa wilaya ya Mbulu, Veronica Kessy .


Akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo mwaka 2024, Kessy alipongeza Taasisi ya Chem Chem ambayo imewekeza wilaya ya Babati katika shughuli za Utalii na Uhifadhi kuendeleza michezo kupitia uhifadhi mkoa Manyara.


"Tunawapongeza Chem Chem kwa kuendeleza michuano hii kila mwaka ambayo inalenga kuendeleza uhifadhi wa mazingira na kupiga vita vitendo vya ujangili"alisema


Alisema serikali inathamini mchango wa Chem Chem katika kuendeleza uhifadhi na akawataka wananchi wa wilaya ya Babati kuendelea kushiriki katika uhifadhi kwani Kuna faida kubwa zinapatikana.


Meneja Mkuu wa Chem Chem, Clever Zulu alisema Chem Chem itaendelea kudhamini michezo hiyo ili kuongeza uewelewa katika masuala ya uhifadhi.


Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ya michuano hiyo ni "Tunza Mazingira Okoa Twiga"na wanatarajiwa mamia ya wakazi wanaoishi katika vijiji 10 ambavyo vinaundwa hifadhi ya jamii ya wanyamapori Burunge watashiriki.


Katibu wa michuano hiyo John Bura alisema timu 35 zitashiriki michuano hiyo, ambayo timu 18 za wakubwa za soka, timu 9 za vijana chini ya miaka 18 na timu 8 za wanawawake.


Bingwa wa soka mwaka huu atapewa zawadi ya kikombe na fedha taslimu Shilingi million 2.5, wa pili millioni 1.5, wa tatu 1 millioni na kwa wanawake bingwa 1.5 millioni, wa pili pili 1 millioni na wa Tatu 500,00


"Kwa timu za vijana mshindi wa kwanza millioni Moja, wa pili 600,000 na mshindi wa tatu 400,000 pia mabingwa wote watapewa medali na pia kutakuwa na zawadi za wachezaji Bora"alisema


Afisa wanyamapori wilaya ya Babati, Christopher Laizer alisema lengo la michuano hiyo ni kuhamasisha utunzwaji mazingira, kutoa elimu juu ya uhifadhi,kupiga vita ujangili, kujenga mahusiano katika Jamii na kuimarisha afya za wadau.


Mwisho



No comments: