VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYATAKIWA KUJENNGA MIUNDOMBINU YA MICHEZO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday 15 September 2024

VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VYATAKIWA KUJENNGA MIUNDOMBINU YA MICHEZO

 



Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


VYOMBO vya Ulinzi na Usalama nchini vimetakiwa kuendelea kujenga miundombinu ya michezo, ikiwa ni pamoja na kuwa na viwanja vya mpira wa miguu vyenye viwango vya kimataifa.


Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma, alitoa wito huo mkoani Morogoro wakati akihitimisha Mashindano ya 15 ya Michezo ya Majeshi ya Ulinzi na Usalama,


Aidha Naibu Waziri Mwinjuma alisema tayari mazungumzo yameanza kufanyika kufanikisha dhima ya wachezaji wanaotoka katika Majeshi kuwakilisha Taifa mashindano mbalimbali ya Kimataifa


Aidha aliviomba vyombo hivyo vya Ulinzi na Usalama kuendelea kushirikiana na Wizara hiyo ya utamaduni na vyama vingine vya Michezo nchini kuweka taratibu ambazo zitawezesha Majeshi kuendelea kutoa washiriki wengi watakaowakilisha Taifa kwenye mashindano hayo ya Kimataifa.


Alisema "Nimevutiwa sana na jinsi wanajeshi walivyoonyesha  nidhamu wakati wote wa mashindano pamoja na ukakamavu hata kwenye michezo,".


Mnadhimu Mkuu wa  Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Salum Haji Othman alisema  michezo hiyo inaumuhimu kwa wanajeshi hao kwani inaimarisha afya na akili kwao


Alisema dhumini la uwepo wa michezo hiyo ni kuimarisha afya na akili ili waweze kufanya kazi vizuri za kulinda raia.


Mashindano ya michezo ya Majeshi (BAMMATA) ya mwaka 2024, Timu Kanda ya Ngome imeibuka Bingwa wa Jumla kwa kujinyakulia vikombe vingi.


Mwisho.

No comments: