Wafanyabiashara Manyara Watakiwa Kutotumia vipimo batili - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday 10 September 2024

Wafanyabiashara Manyara Watakiwa Kutotumia vipimo batili

 

Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoani Manyara Dennis Misango akizungumza na Mwandishi wa Maipac Media




Na Epifania Magingo,Babati


maipacarusha20@gmail.com 


Wafanyabiashara Mkoani Manyara wametakiwa kuacha kutumia vipimo batili pindi wanapofanya manunuzi ya mazao mbalimbali kutoka kwa wakulima kwakuwa kutumia vipimo hivyo ni kosa la jinai.


Kutumia vipimo batili visivyothibitishwa na wakala wa vipimo katika ununuzi wa mazao hakumnufaishi mkulima kwa thamani ya gharama alizotumia kuzalisha mazao bali ni kuwawezesha wafanyabiashara walaghai kujinufaisha na kumlangua.


Akizungumza na Mwandishi wa Maipac Media ofisini kwake Meneja wa Wakala wa Vipimo Mkoani Manyara Dennis Misango amesema wakulima wanapaswa kutumia vipimo sahihi wakati wa kuuza mazao yao ili kupata thamani ya fedha sahihi kwa uzito wa mazao yaliyouzwa.


"Wakulima tumekuwa tukilalamika mara kwa mara kwamba ukiangalia nguvu iliyotumika kulima mazao na nguvu ya kuvuna,umevuna vuzuri lakini thamani ya pesa ulioipata kulingana na yale mazao uliouza inakua ni ndogo, thamani ile inakua ndogo kwasababu ulikubali kuuza yale mazao kwakutumia vipimo batili".


Aidha, amesema wakulima wanapaswa kuwauzia mazao yao wafanyabiashara ambao wanaotumia  mizani iliohakikiwa na wakala wa vimipo kwakua itasaidia kumnufaisha mkulima huyo kwa kuiyona thamani ya fedha kulingana na mazao aliyouza.


"Tusikubali kuuza mazao yetu kwa kutumia vipimo batili, bali tuuze kwa kutumia vipimo sahihi,tusikubali kuibiwa, unapoyauza mazao yako kwa vipimo batili maana yake umekubali kuibiwa".


Hata hiyo, Misango amesema vipimo batili ni vipimo ambayo havijahakikiwa na wakala wa vimipo Tanzania ambavyo vinatumiwa katika sekta ya biashara huku akibainisha vipimo batili kuwa ni ndoo, visado, mabakuli, vikombe kwakua havina vigezo kwamujimbu wa Sheria ya vipimo.


Amesema mazao yote ya shambani yanapaswa kuuzwa kwa uzito usipopungua kilogramu 100 hadi 105 huku akitaja kuwa matokeo ya lumbesa kutoka kwa wafanyabiashara inataokana na kutumia vipimo batili.


Kwa mujibu wa Sheria ya vipimo sura namba 340 kifungu Cha 35 kinaeleza kuwa mtu yeyote haruhusiwi kuwa na kipimo batili katika eneo lake la biashara kwakua ni kosa kisheria na anakuwa ametenda kosa la jinai.

No comments: