WAFANYAKAZI WASIMAMIZI WA MELI NA BANDARI WAELEZA KUTO ATHIRIKA NA MABADILIKO YA MWEKEZAJI,HALI NI SHWARI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday 2 September 2024

WAFANYAKAZI WASIMAMIZI WA MELI NA BANDARI WAELEZA KUTO ATHIRIKA NA MABADILIKO YA MWEKEZAJI,HALI NI SHWARI

 



Na Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com 


LICHA ya mabadiliko yaliyojitokeza kafika usimamizi wa shughuli za kutoka chini ya Mamlaka ya Bandari nchini(TPA) na sasa mwekezaji mpya DP World ya nchini Dubai, wafanyakazi wa shughuli za usimamizi wa Meli na bandari wamesema hadi sasa mabadiliko hayo hayajawaathiri kwa namna yoyote ile na hali kwa wafanyakazi ni shwari.


Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari, DOWUTA, Muharami Manyara alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro baada ya kufanyika kwa mkutano wa 36 wa Baraza kuu la wafanyakazi.


Muharami alisema wafanyakazi na chama hicho wako katika hali ya Amani na Utulivu  na kwamba kupitia shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini TUCTA, Menejimenti na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, wanaamini mchakato wowote utaendelea kuwa shirikishi na haki za wafanyakazi zitaendelea kulindwa sambamba na mahusiano mazuri baina ya mwajiri na mfanyakazi.


"Usimamizi wa Meli na Bandari ulikuwa na waajiri watatu MCCL kwa Upande wa Marine ambapo changamoto zilizopo zinaendelea kutatuliwa na Serikali ya pili ni TICTS lakini sasa inaitwa Tanzania East Africa Gateway Terminal L.T.D, halikadhalika TPAambayo ndio tumepata mabadiliko na yakasemwa mengi lakini sasa tunashukuru tunakwenda vizuri, na tayari kampuni ya DP world imeshaanza kazi, na wafanyakazi wa TPA wamehamia DP world bila matatizo yeyote na kuna Utulivu wa hali ya juu" alisema Mwenyekiti huyo wa DOWUTA.


Muharami akasema kwa sasa wanaendelea na mazungumzo yanaendelea kati ya Chama na mwajiri huyu mpya DP world ili kufungua tawi jipya la chama cha Wafanyakazi na makusudi yao ni kuongeza zaidi ya wanachama.


Alisema awali baada ya kuja kwa mwajiri mpya aliyeanza shughuli zake za uendeshaji bandarini Aprili 07 mwaka huu, walitoa fursa kwa wafanyakazi wanaotaka kuajiriwa na DP world kwenye mchakato huru na usio na shuruti na walioshindwa walipewa maslahi yao stahik kwa mujibu wa mkataba wa ajira.


Akasema Mkutano wa Baraza hilo la wafanyakazi ni Mkutano halali wa Kikatiba ambalo hufanyoka kila mwaka mbao pamoja na mambo mengine mafanikio na changamoto za kwenye matawi pamoja na mwenendo mzima wa chama, taratibu na wapi wanakwenda na wanayojadili ni pamoja na masuala yanayohusu kazi, wafanyakazi na tija mahali pa kazi.


"Inawezekana kwenye kazi zetu tunaweza kukutana na changamoto, vikwazo na vitu vingine, lakini kwa sasa niwe muwazi, tunakwenda vizuri kichama, kitaasisi na katika Uongozi wetu"Alisisitiza Muharami.


Naye Mwenyekiti wa DOWUTA bandari ya Dar es salaam Bw Mashaka Karume, Allsema utulivu uliopo kwa sasa bandarini hapo umechangiwa na elimu iliyokuwa ikitolewa kwa wafanyakazi kuhusu mabadiliko yaliyofanyika


"Kwa kituo cha Dar es salaam Hadi sasa hali ni shwari, ikumbukwe  tangu Januari mwaka huu hadi sasa tulikuwa na pilika za ubinafsishaji Kati ya DP world na TPA, lakini tunamshukuru Mungu Menejimenti na chama cha wafanyakazi  tulifanya jitihada za makusudi kuhakikisha hali ya utulivu inakuwepo kiwandani, na Hadi sasa Hali bado  ni tulivu"Alisema Mshaka Karume,mwenyekiti wa dowuta,bandari ya dar es salaam.


Akasema changamoto pekee iliyoonekana ni Ugeni wa mambo ikiwemo mwajiri mpya lakini kwa kushirikiana  walijitahidi kutoa elimu kwa wafanyakazi kabla ya ubinafsishaji Ili Kila mfanyakazi aelewe mwajiri huyo ni nani, atakayebaki TOA atapata maslahi Gani ma anayekwenda DP world atapata maslahi Gani ambapo wafanyakazi zaidi ya 200 walikubali kwa hiyari kwenda kwa mwajiri huyo mpya na wapo hadi sasa huko huku waliobaki TPA kukiwa hakuna aliyepotea maslahi na mwajiri anaendelea kuwapangia majukumu.


"Waliohamia DP world Huwa kuna utaratibu wa kiutumishi ukikoma ajira kutoka kwa mwajiri mmoja, nao maslahi yao yote yalizingatiwa kwa kupata haki zao zote  Hadi pale alipokuwa ametumikia ajira yake kwenye eneo hilo kwa mujibu wa mkataba wa hali Bora ya kazi na Kila mmoja alifurahia.


Kwa mujibu wa Mwakilishi wa menejimenti ya mamlaka ya usimamizi wa bandari aliyejitambulisha kwa jina Moja la Mwajuma, alishukuru ushirikiano ambao wameendelea kuupata kutoka kwa wafanyakazi kupitia DOWUTA na makubaliano mbalimbali ambayo wameendelea kuafikiana ikiwemo.mkataba wa Hali Bora kwa wafanyakazi na kupata kanuni za mabaraza ya wafanyakazi.


Akasema utulivu uliopo sasa umekuwa tukisaidia tija ya utendaji Kazi ambapo mchango unaofanywa na wafanyakazi hatuwasaidii wao binafsi bali pia taasisi na Taifa kwa ujumla.


"Mamlaka ya usimamizi wa bandari utaendelea kushirikiana na wafanyakazi wakati wote, wito wangu Kwa wafanyakazi ni kuendelea kushirikiana, kushikamana, kuwa na uadilifu na uwajibikaji wakati wote"alisisitiza Mwajuma.


Mwisho.

No comments: