Wakazi Babati waiomba Tume huru ya Uchaguzi kuboresha mifumo ili kuepusha foleni - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 4 September 2024

Wakazi Babati waiomba Tume huru ya Uchaguzi kuboresha mifumo ili kuepusha foleni

 




Na Epifania Magingo, Babati 


maipacarusha20@gmail.com 


Wakazi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara wameiomba Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi inayoshughulika na  zoezi la uwandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura kuboresha mfumo wa uboreshaji wa taarifa za muandikishwaji ili kuepusha foleni ya kukaa kwa muda mrefu kwenye vituo hivyo.



Zoezi la uboreshaji wa daftari hilo litadumu kwa muda wa siku Saba ambapo  limeanza September 4, na kutarajiwa kumalizika September 10 ambapo kumeonekana kuwa na muitikio mkubwa wa wananchi kujitokeza kijiandikisha na kuboresha taarifa zao.


Wakizungumza wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura baadhi ya wakazi wa Mji wa babati akiwemo  John Nzwalile amesema ipo faida ya kuboresha taarifa kwa Kila mmoja kwakua itasaidia kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi Muda ukifika,huku Nuru Omar ambaye hakuwahi kujiandikisha kwasasa amefisha umri wa kujiandikisha amewaomba Vijana waliokidhi vigezo kujitokeza kwenye vituo na kujiandikisha.


"Kunafaida ya kuboresha daftari kwasababu utashiriki kwenye chaguzi zote kwakua unatengeneza Serikali na Kila mwananchi anahaki ya kujiandikisha,Mimi nimejitokeza na wengine wajitokeze kwa wingi kwakua zoezi Hilo ni la Muda mfupi.".


Naye,Afisa Uandikishaji wa Jimbo la Babati Mji,Edna Moshi wakati akizungumza kwenye moja ya kituo Cha uandikishaji amesema kuwa kumejitokeza changamoto ya mtandao umekua ukichukua mda mrefu kwa mteja mmoja wakati inachukua taarifa kwa mboreshwaji. 


"Kwaio tumewasiliana na tume ya Taifa ya Uchaguzi na kwabaadhi ya vituo wameshakifanyia kazi na changamoto hii imeenza kupungua na tutaendelea kufanyia kazi changamoto zingine ili kuhakikisha kwamba huduma hii tunaitoa kwa uharaka ili watu wasikae kwenye vituo kwa mda mrefu".


Imeelezwa kuwa kwa Mkoa wa Manyara zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura linaendelea kufanyika kwenye Wilaya tatu za Mkoa huo ambazo ni Babati, Mbulu na Hanang.

No comments: