DC KAGANDA AZINDUA UJENZI SHULE YA WAVULANA MWADA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday 30 October 2024

DC KAGANDA AZINDUA UJENZI SHULE YA WAVULANA MWADA





 Na: Epifania Magingo,Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Mkuu wa Wilaya ya Babati  Emmanuela Mtatifikolo Kaganda  amezindua ujenzi wa Shule ya Bweni ya Wavulana inayojengwa katika kata ya Mwada, Kijiji cha Ngoley Halmashauri ya Wilaya ya Babati kwa kuchimba msingi wa madarasa ya Shule hiyo.


Ujenzi wa Shule hiyo ya Bweni ya Wavulana kwa Mkoa wa Manyara wilaya ya Babati ni Miongoni mwa Shule saba za Kanda zinazojengwa hapa nchini kwa kipindi cha mwaka 2024/2025 kupitia mradi wa SEQUIP fedha zilizopokelewa katika Shule mama ya Sekondari Mbungwe.


Akizungumza katika uzinduzi wa ujenzi wa shule hiyo Mkuu wa Wilaya ya Babati Kaganda ameeleza kuwa ndani ya Wilaya ya Babati Shule hiyo itakua ya pili kubwa kupokea fedha nyingi ikiwa ni pamoja na Shule ya Wasichana iliyojengwa katika halmashauri ya Mji na kufanya jumla ya shule zote mbili wilaya kupokea Bilioni Nane za ujenzi wa Shule hizo huku akiwataka wananchi kushikamana ili kufanikisha malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakitari Samia Suluhu Hassan.


"Shule hizi zinajengwa nchi nzima ni bilioni za fedha ambazo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezitoa kwaajili ya kuboresha na kufanya mageuzi makubwa kwenye sekta ya Elimu ndani ya nchi yetu, Sisi Mkoa wa Manyara na Wilaya ya Babati tumepewa Heshima kubwa Sana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkoa huu ameleta fedha za kujenga Shule mbili ya Wasichana, Shule ya Sayansi na Shule hii ya Wavulana ni upendo mkubwa sanaa" .


Aidha,Kaganda amewataka viongozi kushikamana ili mradi huo uweze kukamilika kwa haraka ifikapo Januari 2026 wanafunzi waanze kutumia madarasa hayo, huku akimtaka Mkandarasi kusimama vizuri katika nafasi yake Mradi uweze kutekelezwa kwa viwango vinavyostahili.


Kwa upande wao wananchi wa Kata ya Mwada wameonesha kufurahishwa na ujenzi wa Madarasa hayo pamoja na Mabweni na kukiri kuwa usumbufu utaisha na watoto wao wataosoma katika maeneo mazuri, halikadhalika itafanya maendeleo ya kijiji kuongezeka kwa kasi.

No comments: