Na Prisca Libaga Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Longido tarehe 15.10.2024 imetoa elimu kinga dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa wanafunzi 405 wa Shule ya Msingi Namanga na Wanafunzi 803 wa Shule ya Sekondari ya Namanga katika eneo la mpaka, Kata ya Namanga wilayani Longido Arusha (M).
Wanafunzi hao walihamasishwa wakatae dawa za kulevya ili waweze kutimiza ndoto zao za kielimu.
Pia, walihimizwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa za kulevya kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment