DKT.TAX AZINDUA MRADI WA MAJI WENYE THAMANI YA TSHS. BIL.1.4 TANDAHIMBA. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 7 October 2024

DKT.TAX AZINDUA MRADI WA MAJI WENYE THAMANI YA TSHS. BIL.1.4 TANDAHIMBA.




Na Mwandishi Wetu 


maipacarusha20@gmail.com 


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe.Dkt. Stergomena Lawrence Tax amezindua mradi wa Maji Chitoholi uliopo katika Kata ya Mkundi Wilaya ya Tandahimba Mkoani Mtwara.


Dkt. Stergomena amezindua mradi huo leo Tarehe 7 Octoba 2024, wakati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi Mkoani Mtwara ambayo inaambatana na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi kupitia mikutano ya hadhara.


Mradi huo unakusudiwa kutoa huduma katika vijiji sita vilivyopo katika Kata za Mkundi na Chikongola, vyenye watu wapatao 10,817 ikiwa sawa na asilimia 4 ya Wananchi wa Tandahimba. 


Katika salamu zake kwa Wananchi wa Vijiji hivyo waliofika kushuhudia uzinduzi huo, Dkt.Tax ameeleza dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kuwa wananchi wanafikiwa na huduma ya maji katika maeneo yao.


"Mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amedhamiria kumtua mama ndoo, niwahikikishie kuwa juhudi zake zitaendelea ili kuwaondolea wananchi adha ya upatikanaji wa maji kote nchini" amesema Dkt.Tax 


Awali akitoa maelezo ya mradi huo kwa Mhe.Waziri, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Tandahimba Mhandisi Antidius Muchunguzi amesema kuwa unatoa uhakika wa Maji Safi na Salama kwa muda wote.


Ameeleza manufaa mengine ya mradi huo kuwa ni kupunguza magonjwa yanayosababishwa na maji yasiyo safi na salama, akina mama kutumia muda wao mwingi kwenye kazi za uzalishaji mali badala ya kutafuta maji.



No comments: