Na Epifania Magingo Babati, Manyara
maipacarusha20@gmail.com
Kamati ya Wataalamu iliyoundwa kuchunguza chanzo cha kutokea maporomoko ya udongo, mawe na tope katika mlima Hanang' imebaini kuwa chanzo kilikuwa mipasuko ya miamba iliyohifadhi maji ya mvua iliyonyesha mfululizo kushindwa kuhimili na kusababisha udongo kuanza kuserereka na kuleta maafa kwa wananchi .
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa huduma za Jiolojia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania( GST) Dakitari Ronald Massawe wakati akitoa ufafanuzi wa matokeo ya utafiti wa kamati ya wataalamu iliyoundwa na kitengo cha maafa ofisi ya Waziri Mkuu na kuwasilishwa kwa wataalamu wa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang.
"Kwenye ule mlima kule juu kuna structures kubwa eeh na nyingine ndogo sasa eeh izo ndogo ndogo mvua zinapenyesha maji yanaenda kujihifadhi mle,kwaio kuna Lea ndogo sana ya udongo lakini miamba nayo imechanika ikahifadhi hayo maji kuanzia kwenye structures ndogo na kubwa (miamba liovunjika ) Matokeo yake sasa unafika mahali ule mlima unashindwa kuhimili basi ikitokea sistabansi hata kidogo basi unaserereka kwa sababu maji yanalainisha miamba".
Amesema mlima Hanang ni miongoni mwa milima iliyopo katika mkatiko au ufa wa Balanginda wa ukanda wa kaskazini wa bonde wenye miamba yenye mipasuko mingi inayohifadhi maji ambayo siku chache kabla ya kutokea maporomoko ya Disemba 3 mwaka 2013 ilijaa maji kutokana na mvua zilizonyesha mfululizo iliyosababisha kumeguka na kuanza kuserereka na kusababisha maafa.
"Taarifa yetu hii inashauri kwasababu tumeshaiwasilisha kwa mkuu wa Mkoa, kwenye Halamshauri ya Hanang' wanachukua sasa action manake wanachukua hatua ya kwenda kuyafanyia kazi Yale yote ambayo tumeyashauri kupitia ile taarifa na tunatoa rai kwa maaneo yake ambayo yalitokea maafa ili kuzuia Tena hili jambo kutokea wakati mwingine".
Mkuu wa Wilaya ya Hanang Almish Hazali à metoa pongezi na kushukuru kwa utolewaji wa taarifa hiyo ambayo amesema imeleta mwanga unaoweza kusaidia kuelimisha wananchi na kwamba Serikali inaendelea kuangalia tatizo hilo na kushughulikia kwa haraka.
"Kwaio tunatakiwa kuwa makini mda wote,Yani tujihadhari na tuko tayari kutoka Elimu kwa wananchi na pia tutajitajidi kuotesha miti mana maneno ambayo hayana miti yameleta adhari Katika maeneo hayo".
Uwasilishaji wa ripoti hiyo ya utafiti wa chanzo cha maporomoko ya udongo na mawe kutoka mlima Hanang' imeenda sambamba na uzinduzi wa nyaraka ya usimamizi wa maafa, ambapo Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Maafa Dakitari Jim Yonaz aliyekuwa Mgeni Rasmi ameelekeza wataalamu wa Halmashauri ya Hanang kuzingatia ili kusaidia kupunguza athari ya maafa kwa siku sijazo.
"Leo tumefanya tathimi ya maafa yaliyotokea na hiyo yote imetusaidia Serikali kupata uelewa, tunamshukuru kupata ripoti ya tathimi hiyo,tumezindua nyaraka mbalimbali za kutuongoza
Namna ambavyo kamati itakavyokabiliana na maafa kwa wilaya ya Hanang' namna itafanya kazi"
Inaelezwa kuwa ripoti ya kina ambayo tayari imezinduliwa ilifanyika April 2024 na kukamilika Mei 2024.
No comments:
Post a Comment