Majengo FC kuvaana na Bodaboda FC fainali chemchem CUP 2024 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 16 October 2024

Majengo FC kuvaana na Bodaboda FC fainali chemchem CUP 2024

 







Na: Mwandishi wetu, Maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Babati. Timu ya majengo Fc inatarajiwa kuchuana na Bodaboda FC katika fainali ya Chemchem CUP 2024, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa Manyara Qeen Sendiga.


Fainali hiyo itachezwa uwanja wa Mdori wilayani Babati mkoani Manyara Octoba 20, mwaka huu.


Majengo imefanikiwa jana kutinga fainali baada ya kuicharaza timu ya Mdori FC magoli 4-0.


Bodaboda FC imefanikiwa kutinga fainali baada ya kuwang'oa mabingwa watetezi Macklion FC goli1-0.


Mratibu wa michuano hiyo, John Bura alisema jana kuwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa mkoa wa Manyara, Queen Sendiga.


Maandalizi yote muhimu yamekamilika ambapo katika michezo mingine kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17, Mawezi FC inatarajiwa kuchuana na Olasiti FC.


Kwa upande wa wanawake Mdori FC tayari imetinga fainali na itapambana ma Olasiti FC


Jumla ya timu 35 zilishiriki katika michuano ya Chem chem CUP mwaka 2024 ambayo imegharimu  takriban sh  78 milioni.


Michuano hiyo ya 10  imedhaminiwa na Taasisi ya Chem Chem ambayo imewekeza wilaya ya Babati katika eneo la hifadhi ya Jamii ya Burunge kufanya  shughuli za Utalii na Uhifadhi.



Meneja Mkuu wa Chem Chem, Clever Zulu amesema lengo la michuano hiyo ni kuhamasisha uhifadhi wa wanyamapori na kupiga vita ujangili.



Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ya michuano hiyo ni "Tunza Mazingira Okoa Twiga" na wanatarajiwa mamia ya wakazi wanaoishi katika vijiji 10 ambavyo vinaundwa hifadhi ya jamii ya wanyamapori Burunge watashiriki katika michezo ya fainali.


Mwenyekiti wa michuano hiyo, Erasto Belela alisema timu 35 zimeshiriki michuano ya mwaka huu, ambayo timu 18 za wakubwa za soka, timu 9 za vijana chini ya miaka 18 na timu 8 za wanawawake.


Belela alisema bingwa wa soka mwaka huu atapewa zawadi ya kikombe na fedha taslimu sh million 2.5, wa pili millioni 1.5, wa tatu 1 millioni na kwa wanawake bingwa 1.5 millioni, wa pili pili 1 millioni na wa Tatu 500,00


"Kwa timu za vijana mshindi wa kwanza millioni Moja,wa pili 600,000 na mshindi wa tatu 400,000 pia mabingwa wote watapewa medali na pia kutakuwa na zawadi za wachezaji Bora"alisema


Mwisho

No comments: