Naibu Waziri Sillo Awaasa wazazi kuzungumza na watoto KUJIEPUSHA na VITENDO viovu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 8 October 2024

Naibu Waziri Sillo Awaasa wazazi kuzungumza na watoto KUJIEPUSHA na VITENDO viovu

 





Na Mwandishi Wetu Maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Daniel Sillo amewaasa wazazi na walezi kuzungumza na watoto wao kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo maisha yao kwa uwazi mkubwa ili kuwaokoa wasiingie kwenye mambo mabaya yasiyofaa katika jamii.


Naibu waziri Sillo ameyazungumza hayo katika mahafali ya kidato cha nne kwenye shule ya Sekondari Matufa iliyopo kijiji cha Matufa, kata ya Magugu, Tarafa ya Mbugwe, Wilaya ya Babati na kusisitiza kuwa wazazi na walezi wameacha majukumu yao ya msingi hali inayopelekea vijana kujiingiza kwenye matendo ya ukatili wa kijinsia na kuhatarisha usalama wa jamii.


“Ninaomba sana wazazi tusikimbie majukumu ya msingi ya kuongea na vijana wetu, tunalaumu watoto wa siku hizi kwakuwa na wao wametokana na wazazi wa siku hizi, unaposikia kijana mdogo wa miaka 25 amembaka bibi kizee, sisi tupo wapi na tunajitengaje na hiyo dhambi? Kwahyo nawomba wazazi zungumzeni na vijana kwa uwazi mkubwa”.


Kwa upande wake diwani wa Viti Maalumu Kata ya Magugu Naomi Richard Sangu amewasihi vijana kutumia nguvu kazi waliyonayo kujiletea maendeleo na kuacha kufanya vitendo vya ukatili na badale yake wasimamie lengo kuu la kujitafutia maisha yao ili wakuze uchumi wao pamoja na wa jamii kwa ujumla.


“Niwaase vijana waache maramoja tabia hii mbaya na wasimame katika lengo la kutafuta maisha ili na wao wapande kiuchumi na masiha yao yaendelee kuwa sawa”.


Shule ya sekondari Matufa ni shule ya Serikali yenye jumla ya wanafunzi 174 ambayo ilianzishwa 2019 ilijengwa kwa lengo la  kutatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu ambapo awali walikua wanakwenda Shule ya sekondari Magugu lakini pia kuwasaidia kuepuka matendo ya kikatili kwenye njia wanazopita.

No comments: