RC SENDIGA AJIANDIKISHA KUPIGA KURA, AHIMIZA WANANCHI MANYARA KUJITOKEZA KWA WINGI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 11 October 2024

RC SENDIGA AJIANDIKISHA KUPIGA KURA, AHIMIZA WANANCHI MANYARA KUJITOKEZA KWA WINGI

 





Na Epifania Magingo,Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Manyara kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la uandikishwaji wa daftari la Mkazi ikiwa ni maandalizi ya kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika  Novemba 27 mwaka huu.


Zoezi la uandikishwaji wa daftari la wakazi la mpiga kura limeanza 11 Octoba hadi 20 actoba àmbapo Kila mwananchi anahaki ya kikatiba kujitokeza kwenda kujiandikisha kwa lengo la kupiga kura.


Hayo ameyazungumza wakati alipojitokeza kwenye  kituo Cha kujiandikisha Mtaa wa mrara kata ya Babati Mkoani Manyara na kusema kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni muhimu na ndio mwanzo na uundaji wa Serikali ambayo inategemewa kuanza kufanya kazi katika msimu wa miaka mitano inayokuja.


"Ninawahamaisha kule mliko mtoke mje mjiandikishe,kazi ya kujiandikisha sio kubwa chukua mda wako kidogo na sie kama Mkoa tumejipanga kuhakikisha kwamba wananchi wote wanafika kituoni wanajiandikisha,Muda wa kujiandikisha Bado ni mrefu tu,twendeni mkikosa tarehe 11 basi tarehe 13 mkajiandikishe".


Aidha, Sendiga amesema Moja kati ya sifa za mwananchi kwenda kujiandikisha katika daftari la wakazi la mpiga kura awe Mkazi wa eneo husika huku akiwa ametimiza umri wa miaka 18 na Zaidi.


"Ukiwa mkaazi tayari unasifa ya kupiga kura,mda ukifika utachagua Mwenyekiti wako wa Kijiji, Mwenyekiti wa kitongoji wa Mtaa unaoishi".

No comments: