TASAF YAKAGUA MIRADI SONGEA NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANANCHI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 7 October 2024

TASAF YAKAGUA MIRADI SONGEA NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

 





Na Mwandishi Wetu,Songea


maipacarusha20@gmail.com 


Mkurugenzi mtendaji wa mradi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii(TASAF) Shedrack Mziray Pamoja na menejimenti wamefanya ziara ya kukagua miradi ya standi mbili Pamoja na ujenzi wa nyumba za waganga sambamba na kisima cha maji  katika halmashauri ya Wilaya ya Songea.


Mziray alisema huo ni utaratibu uliowekwa na menejimenti yake kutembelea miradi inayosimamiwa na Tasaf ili kuona ukamilifu wake na kusikiliza malalamiko ya walengwa wa kaya maskini kwa waliotolewa kwenye orodha kama yapo ingawa alionyesha kutokuwepo kwa malalamiko mpaka sasa.


“Sisi kama menenjimenti ya Tasaf tunao wajibu wakuhakikisha miradi inatekelezwa kikamilifu”


Alisema baadhi ya mambo wanayoangalia cha kwanza kama mnavyofahamu kati ya walengwa tunaohudumiwa ni zaidi ya 1.3  tulifanya tathmini tukaona kuna walengwa Zaidi ya laki 3 na tisini nane (394,000/=) ambao Maisha yao yamebadilika kwa maana sasa  wanaweza kuendelea na Maisha yao bila msaada wa Tasaf.


Mkurugenzi huyo alisema wametembelea na kuangalia kama kuna malalamiko yoyote na namna gani mkoa pamoja na halmashauri wanashughulikia malalamiko yao ambapo katika kijiji cha Parangu kuna walengwa Zaidi ya 60 ambao wametolewa kwenye mpango lakini hakuna malalamiko yoyote.


Pia Mziray alitoa wito kwa mkurugenzi kama kuna maeneo yoyote kuna mwananchi hakutendewa haki inabidi wajiridhishe kama anastahili kuwepo kwenye orodha ya wanufaika.


“Kama kuna meeneo yoyote mwananchi anadhani labda hakutendewa haki basi wao wenyewe wajiridhishe kama kweli mwananchi huyo  anastahili kuendelea kuwepo katika kaya”alisema


Vilevile aliwahimiza wasimamizi wa standi ya Lundusi na Parangu kuongeze juhudi katika usimamizi wa miradi kwasababu haitakiwi ichukue muda mrefu.


Wamewekeana  mikakati na mkurugenzi ya muda wa kukamilisha miradi hiyo ambapo wamekubaliana mpaka mwezi Novemba mwaka huu mradi huo uwe umekamilika, kwasababu Changamoto ya upatikanaji wa fedha imetatuliwa fedha zote zinakuja kwa wakati.


“Tumepeana tarehe za kuhakikisha kwamba nini wakifanye na tarehe zitakapofika basi tutarudi tena kukagua kuona  miradi na kuhakikisha imekamilika”alisema.


“Tumekubaliana na wakurugenzi wasimamizi kwa ujumla kwamba ifikapo  mwezi wa 11  standi hizi 2 ziwe zimekamilika”alieleza


Mratibu wa Tasaf Halmashauri ya Wilaya ya Songea Hossana Ngunge alianza kwa kuishukuru serikali na Tasaf kwa miradi hiyo na kuelezea gharama zilizotumika kukamilisha ujenzi wa nyumba 2 na kisima kirefu na matundu 6 ya vyoo.


Alisema sh milioni 154 imetumika katika ujenzi wa nyumba mbili (2) za wauguzi, matundu sita (6) ya vyoo na kisima kirefu,na ujenzi wa standi ya Kijiji cha Lundusi wamepata zaidi milioni 600 na stand ya Parangu wamepata zaidi ya milioni 300.


Vilevile Ngunge ameeleza changamoto wanazokutana nazo katika kusimamia miradi hiyo.


Alisema changamoto  kubwa ni suala la mfumo kwasababu hizo hela zinatumika ngazi ya halmashauri  wakati mwingine mfumo bank kuu huwa unasumbua inaweza kukaa  miezi 2 au 3 banki kuu hawajafungua kwahiyo kidogo inatuletea shida hasa kwa wale wazabuni wanaoleta mahitaji yao kuwalipa kwa wakati.


Naye mwenyekiti wa Kijiji cha Parangu Benadetha Mapunda ambaye ni msimamizi wa mradi wa ujenzi wa standi ya Parangu alitaja sababu ya kuchelewa kwa mradi huo kukamilika mpaka sasa.


Pia alithibitisha kutolewa kwa baadhi ya  wanufaika wa Tasaf  na kusema kuwa waliotolewa hawajaonewa na ameomba kwa wale wenye mazingira magumu ambao waliachwa kipindi cha nyuma nao wawekwe kwenye orodha ya wanufaika wa mfuko wa Tasaf.


“Wanufaika wa Tasaf ni kweli wametolewa ila hawajatolewa kimakosa ila wametolewa kiuhalali kutokana na serikali inavyopanga”alisema


Sambamba na hilo mratibu wa Tasaf Halmashauri ya wilaya ya Songea Hossana Ngunge alianza kwa kuishukuru serikali na Tasaf kwa miradi hiyo na kuelezea gharama zilizotumika kukamilisha ujenzi wa nyumba 2 na kisima kirefu na matundu 6 ya vyoo milioni 154 ,vilevile ujenzi wa standi ya Kijiji cha Lundusi wamepata zaidi milioni 600 na stand ya Parangu wamepata zaidi ya milioni 300.


Ngunge alieleza changamoto wanazokutana nazo katika kusimamia mradi huo ni suala la mfumo kwasababu hizo hela zinatumika ngazi ya halmashauri  wakati mwingine mfumo banki kuu uwa unasumbua inaweza kukaa  miezi 2 au 3 banki kuu hawajafungua hivyo imekuwa ikileta shida hasa kwa wale wazabuni wanaoleta mahitaji yao kulipa kwa wakati.


Naye mganga ambaye anaishi katika nyumba ambayo ni miongoni mwa miradi iliyosimamiwa na Tasaf Shamsia Wiliam katika zahanati ya kijiji cha Mdundualo alitoa shukrani zake kwa Tasaf na alieleza changamoto waliyokuwa wanakutana nayo kabla ya ujenzi wa nyumba hiyo kuwa walikuwa wanakaa mbali na zahanati, na faida wanazozipata ni pamoja na kutoa huduma kwa urahisi.


“kabla hatujapata hii nyumba hapa tulikuwa tunaishi maisha tupo mbali na zahanati sasa tunashukuru Tasaf walipotupatia nyumba pamoja na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya jambo la kuturahisishia kusogea mahali hapa na tunatoa huduma kiurahisi tofauti na mwanzo na nyakati za mvua ilikuwa ni shida sana sasa hivi ni rahisi kwasababu tupo jirani na kituo”alisema.


Nao wananchi hawakuwa nyuma kutoa shukrani zao kwa Tasaf kwa ajili ya miradi hiyo katika halmashauri yao.


Asante mhagama mkazi wa Kijiji cha Mdundualo anasema kuwa wanashukuru kwa mradi kwasababu unawasaidia sana hasa kwa wajawazito hawapati changamoto ya maji kipindi cha kujifungua


“Kwasisi wanawake tukiwa wajawazito tulikuwa tunateseka sana kwenye huduma ya kliniki kwahiyo sahivi tunashukuru zahanati imeisha na nyumba imeisha  wauguzi wetu wanakaa hapa na haya maji yanatusaidia hata pia kwenye mambo ya leba wengi wanajifungua hapa”


Agnes komba mkazi wa Kijiji cha Lundusi anasema kuwa mradi wa ujenzi wa standi utawasaidia sana,


“kwa kweli mradi tunafurahi kwa kutuletea manufaa yetu hapa usafiri tulikuwa tunaenda mbali kama tunaenda mjini sasa hivi tutakuwa tunapanda hapa hapa jirani na biashara tutanufaika sana


.....

No comments: