Na Mwandishi Wetu, Maipac
maipacarusha20@gmail.com
Mtandao wa Watetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC pamoja na wawakilishi wa Azaki zaidi ya 300 wameendelea na ziara ya kutembelea vyama vya siasa nchini Tanzania kwa lengo la Kusambaza na kukabidhi nakala za ilani ya uchaguzi ya asasi za kiraia ya mwaka 2024/2029
Timu hii ya ziara imefanikiwa kukitembelea Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema CDM Katika ofisi zao zilizopo mikocheni Jijini Dar es Salaam, na kupokelewa na viongozi wao akiwemo ndugu John Mnyika ambae ni katibu mkuu wa chama, ndugu Julius Mwita ambae ni Mkurugenzi wa Mafunzo Tathmini na Ufuatiliaji, Reginald Munisi ambae ni Mkurugenzi wa Mikakati, Susan Lyimo ambae ni Spika wa Bunge la Wananchi , Aron Masuve ambae ni Afisa utawala na Rasilimali na wengine wengi.
Viongozi hawa waliipongeza sana timu kuwa kuweza kuandaa ziara hii muhimu na hasa timu iliyoandaa manifesto kwani imefanya kazi kubwaa sana ya kuwasilisha maoni ya wananchi kwa niaba ya wananchi.
Baada ya kuwasilisha na kujadili kwa kina yaliyomo ndani ya ilani hiyo, Kiongozi wa chama hicho Ndugu John Mnyika alipata nafasi ya kuongea na vyombo vya habari juu ya ilani hii bora na kuelezea umuhimu wa vipaumbele vilivyowekwa katika ilani hiyo vikiwemo, Umuhimu wa katiba mpya, sera ya uchumi jumuishi na maendeleo endelevu, kuheshimu na kutunza haki za binadamu, Utawala wa Sheria na Mgawanyo wa madaraka, kuwepo na uchaguzi Huru na umuhimu wa kulinda mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi na vingine vingii.
Zaidi sana aliweza kutoa maoni yake juu ya ilani hii akisisitiza kuwa upo umuhimu wa ilani hii kuangazia suala la ukuaji wa deni la Taifa na kupanda kwa gharama za maisha kwa wananchi na athari zake
kiuchumi, kwani ni masuala ambayo yanamgusa kila mwananchi na yanaweza kuathiri Tanzania Tuitakayo.
“Mnyika aliongeza kwa kusema kuwa mazingira ya Uchaguzi huru na haki yanaanzia ndani ya katiba na sio katika maneno “
Viongozi hao walimaliza kwa kusisitiza wananchi kwenda kujiandikisha katika daftari la mpiga kura kwani hata kwa wale wenye vitambulisho vya kupigia kura, hawataweza kupiga kura kama hawajajiandikisha katika maeneo yao, akikazia nguvu ya kuchagua viongozi wa kuiongioza tanzania tuitakayo imebebwa na wananchi wenyewe.
No comments:
Post a Comment