Na: Epifania Magingo, Manyara
maipacarusha20@gmail.com
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Manyara kimewahimiza wananchi wenye sifa na nia ya kugombea nafasi za uongozi wa Serikali za Mitaa kujitathimini na kujitokeza kuchukua fomu za kugombea kwa lengo la kupata Viongozi bora na wenye Uzalendo.
Imeelezwa kuwa Uchaguzi ni suala la kitaifa na kwa mujibu wa katiba kila mtanzania anahaki ya kushiriki kwa kujitokeza kujiandikisha katika daftari la makazi kwa eneo husika ili aweze kupiga Kura.
Akizungumza na wanahabari Wilaya ya Babati Mkoani Manyara Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara Peter Toima amesema kuwa
tunapokwenda katika uchaguzi huo ni muhimu kuwapata viongozi wenye elimu vipaji katika Mkoa wa Manyara ili wajitokeze kugombea badala ya kubeza nafasi za uongozi ngazi za mitaa na vitongoji.
"Elimu yako itasaidia njoo gombea katika nafasi hizi ili uingie katika utaratibu wa kuleta maendeleo ya watu kujenga mkoa na kujenga chama".
Amefafanua kuwa, kwa kujibu wa Katiba na ibara ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa ni jambo muhimu wanachama kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la wakazi wa mtaa husika.
"Mkoa wa Manyara una wananchi zaidi ya milioni 2 na wanaishi katika wilaya sita za chama,wilaya 4 za serikali, Halmashauri 7 lakini wapo kwenye vijiji 445 na vitongoji 1,905 ambapo daftari hilo la makazi niko linalokuja nafasi kupiga kura katika kijiji na kitongoji na endapo utakosekana kwenye Daftari ina maana itakosa haki yako ya kupiga kura"Alisema Toima.
Kwa upande mwingine amesema kuwa wanachama wenye nia ya kugombea Chama kinaendelea kujiimarisha hivyo kinataka kubwa na viongozi bora wenye uwezo wa kuwatumikia wananchi.
Aidha, amesema chama hicho hakitakwenda na viongozi wabovu walioshindwa kutekeleza majukumu yao katika kipindi kilichopita cha miaka mitano.
"Umekuwepo katika chama cha Mapinduzi umefanya nini katika chama Mwenyekiti wa kijiji,Diwani hatuko tayari kusonga mbele na viongozi wabovu kwa wale watakaokuwa hawaridhiki watumie kanuni za CCM za uchaguzi kupeleka malalamiko yao".
Zoezi la uandikishaji katika daftari la uchaguzi wa Serikali za mitaa litadumu kwa Muda wa siku kumi na linaanza 11 Oktoba 2024 na uchukuaji wa fomu za kugombea linafanyika tarehe 20 oktoba 2024.
No comments:
Post a Comment