Na Lilian Kasenene,Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
WATU wote wenye nia ovu ya kuharibu zoezi la uandikisha katika daftari la wapigakura kwaajili ya uchaguzi wa Serikali za mitaa, watajalishwa na kwamba hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Adam Malima ametoa tahadhali hiyo jana mjini hapa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na zoezi hilo na uandikishaji wa daftari la wapigakura linaloanza Octoba 11 mwaka huu.
Alisema hadi sasa watu wenye sifa kuandikishwa ni milioni 1,816,485 ambao ni sawa na asilimia 53.2 ya watu milioni 3,414,507 wanaokadiriwa kuwepo mkoani Morogoro kwa mwaka 2024 kutokana na ongezeko la asilimia 3.4 kwa mwaka ambapo idadi ya watu kutokana na sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 ni 3,197,104.
"Sitarajii mtu mwenye akili timamu kuhamasisha watu wasijiandikishe kwenye daftari hili, ni haki ya kila mtu kujiandikisha ili aweze kuchagua viongozi anaowataka" alisema.
Alisema kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya zake wamejipanga vizuri kwaajili ya kuhakikisha zoezi hilo linakwenda kama lilivyopangwa.
Aidha alitaja jumla ya vituo 3,752 vitatumika kuandikisha wapigakura ambapo waandikishaji ni 3998 huku waandikishaji wa 242.
" Tunao waandikishaji wa akiba wa kutosha hivyo ikitokea mwandikishaji yeyote atakiuka au kushindwa kufanya kazi hao watashika nafasi mara moja," alisema Malima.
Hata hivyo alisema vituo vipo katika ofisi za serikali na maeneo mengine ambayo sio majengo ya serikali lengo ni kuwafikia wananchi kwa urahisi.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Khamis Katimba alisema kwa Halmashauri yake inatarajia kuandikisha watu 120,000.
Katimba alisema wameweka mkakati wa kuhamasisha na kutoa elimu kwa watu wenye mahitaji maalumu kupitia matamasha yatakayofanyika Octoba 14 siku ya kumbukizi ya Mwalimu Julius Nyerere.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment