KAMPENI YA NIC KITAA YAZINDULIWA MORO,WANANCHI WATAKIWA KUWA NA BIMA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 13 November 2024

KAMPENI YA NIC KITAA YAZINDULIWA MORO,WANANCHI WATAKIWA KUWA NA BIMA

 




Na: Lilian Kasenene,Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


 

SHIRIKA la Bima la Taifa(NIC) kupitia kampeni yake ya NIC KITAA imewataka watanzania kuhakikisha wanakuwa na bima kwa lengo la kuwaondoa kwenye umasikini pindi wanapopata majanga mbalimbali ya kimaisha.


Kaimu mkurugenzi wa Masoko na mawasilianowa NIC Kafiti Kafiti alisema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya NIC Kitaa katika mkoa wa Morogoro inayotarajia nkuzifikia wilaya zote za mkoa huo.


Kafiti alisema shirika hilo pamoja na kuwa na mtandao mkubwa wa kimkakati lina lengo la kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu ya Bima ikiwa na katika kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan ya kuwa na watu wenye uelewa wa masuala ya bima.


“Mwanachama ama mteja yoyote anapokuwa na bima maana yake ni moja kwa moja anakuwa amejiondoa kwenye hatua za umaskini, unapokuwa huna bima maana yake unajiongezea uwezekano wa kuendelea kuwa maskini leo umepata ajari ,au nyumba kuungua au biashara kukwamba maana yake unarudi nyumba kwa zaidi ya hatua moja,”alisema.


Kaimu huyo mkurugenzi alisema nia nyingine ya kampeni ni kuondoa dhana potofu ya kwamba bima hazisaidiii wananchin jambo ambalo si sahii.


Aidha alisema tayari wamefanya kampeni kwenye mkoa wa Mwanza na wanatarajia kufika kwenye mikoa ya Dodoma,Arusha, Singida na baadaye Zanzibar lengo likiwa ni kumfikia kila mmoja kumpatia elimu kwa undani zaidi kwani shirika hilo lina uwezo mkubwa wa kutoa huduma iliyo bora.


“Shirika hili lina mtaji mkubwa na ina uwezo wa kumuhudimia kila mtanzania kwani tupo nchini kwa zaidi ya miaka sitini(60) na ina viwango vya kimataifa,na wamekuwa wakitoa huduma za bima zaidi ya thelathini, sisi tunasogeza huduma kwa watanzania kuanzia wa hali ya chini, wakiwemo wafanyabishara wadogo, wakulima,”alisema.


Aliwatoa wasisiwasi wateja wao kwa wao akama shirika hawana ubabaishaji katika suala zima la utoaji huduma na kwamba hawamuacho mtanzania yoyote nyuma.


Kwa upaande wake kaimu meneja wa NIC mkoa wa Morogoro Fredrick Solomon alieleza kuwa kampeni hiyo itawafikia wananchi wa wilaya zote za Kilosa, Kilombero, Ulanga, Malinyi, Mvomero, na Gairo.


Mwisho.

No comments: