Na: Mwandishi wetu,Meatu.
maipacarusha20@gmail.com
Tembo aliyekuwa kivutio kikubwa cha Utalii eneo la Ikolojia ya Serengeti kutokana na kuwa na pembe kubwa zaidi ambaye ni maarufu kwa jina la Zito ametoweka.
Habari za kutoonekana Tembo huyo, zilianza kuripotiwa tangu wiki iliyopita na vyombo vya habari kwa mambo ya uhifadhi na kwenye mitandao ya kijamii ya wahifadhi ndani na nje ya nchi.
Tembo huyo kwa mara ya mwisho alionekana akitoka eneo la Serengeti akielekea eneo la Kaskazini mwa pori la akiba la Maswa ambapo kuna kampuni za uwindaji wa kitalii.
Mdau wa Utalii, Julian Peter alisema kwa takriban wiki moja sasa wamekuwa wakimtafuta tembo huyo ambaye ni kivutio cha watalii bila mafanikio.
"Hatuwezi kusema ameuawa na wawindaji wa kitalii au la ila haonekani na alikuwa ni kivutio sana kwa watalii"alisema
Baadhi ya wadau wa Utalii katika eneo la Singita na Serengeti na Meatu walieleza kuwa hakuna uhakika Tembo huyo yupo wapi.
John Mollel alisema kwa kuwa suala hilo bado linafatiliwa na vyombo mbalimbali ila kama atakuwa amewindwa basi ni kihalali.
"Taarifa za mwisho zinaeleza Tembo huyu alitoka Serengeti na kuelekea upande wa mapori la akiba la Maswa wilaya ya Meatu ambapo kuna vitalu vya uwindaji Sasa kama amewindwa ni kisheria "alisema
Mollel alisema kama hatakuwa hajawindwa basi amejificha katika vichaka vikubwa vilivyopo pori la akiba la Maswa
Afisa Wanyamapori wilaya ya Meatu, Joseline Mpelasoka alipoulizwa kuhusiana na taarifa za kutoonekana Tembo "Zito" alisema Hana taarifa.
"Hizo taarifa za Tembo huyu binafsi sina lakini kama zingekuwepo Kuna vyombo vingine vya wizara ya Maliasili na Utalii vinahusika"alisema.
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti inazungukwa na mapori ya akiba ambapo kuna kampuni kadhaa za wawekezaji wa uwindaji wa kitalii.
Mwisho
https://singita.com/2021/07/zito-the-elephant/?fbclid=IwZXh0bgNhZW0CMTEAAR3-U0GySiBpJZCG_jHXYlJvEqAY7IHps0KoXV1LAWNqO0tTYS5DEaw-k-8_aem_96F6zk7dPHUECf4Rm7Lqvw
https://africageographic.com/stories/has-zito-the-cross-border-super-tusker-been-trophy-hunted-in-tanzania/?fbclid=IwY2xjawGPHtFleHRuA2FlbQIxMQABHavf_94tfWJxxYGv3K6putoZGU_SVnXBCimRwYmTmEosUMmFnIOblyN7mA_aem_IXBd6UHvP5KujDPwe8S_VA&sfnsn=wa
No comments:
Post a Comment