MNADA WA SABA RUNALI, TANI 4,003 ZA KOROSHO ZIMEUZWA KWA BEI YA JUU TSH. 3,060/= - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 24 November 2024

MNADA WA SABA RUNALI, TANI 4,003 ZA KOROSHO ZIMEUZWA KWA BEI YA JUU TSH. 3,060/=

 




Na Mwandishi Wetu, Maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Wakulima wa Chama Kikuu cha RUNALI Mkoani Lindi, wameuza Korosho Tani 4,003 kwa bei ya juu ya shilingi 3, 060/= na bei ya chini 2,610/= katika mnada uliofanyika Wilayani Nachingwea leo Jumapili tarehe 24 Novemba 2024.


Mnada huo umefanyika katika ofisi za RUNALI Wilayani Nachingwea,  na kendeshwa na maofisa kutoka soko la bidhaa Tanzania TMX, ambao ndio wenye dhamana ya kusimamia uendeshaji wa minada ya Korosho katika msimu 2024/2025.


Bi.Shanny Mringo ambaye ni Afisa wa TMX ameuelezea mnada huo wa manufaa kwa wakulima, ambao ndio wanaotoa hatma ya kuuzwa au kutokuuzwa kwa Korosho baada ya kikia bei za wanunuzi katika mnada husika.


"Sisi huwa ni wasimamizi wa mfumo wa mauzo, kazi yetu ni kuwaunganisha wakulima na wanunuzi wa Korosho zao, wanaoridhi kuuza ni wakulima wenyewe, na kama mlivyoshudia wakulima wameridhika na bei iliyowasilishwa na wamekubali kuuza" ameeza.


Shaban Issa Mkulima wa Korosho kutoka Wilayani Nachingwea, ameelezea mwenendo wa soko la korosho katika msimu huu, akisema bei bado ni nzuri hata baada ya kufanyika kwa minada sita ya mwanzo.


"Msimu huu bei zipo vizuri, na tumewasikia wataalam kutoka Bodi ya Korosho wakieleza mwenendo wa bei katika soko la Dunia, ukiangalia hata bei ya chini ya mnada huu wa Saba bado ni kubwa kuliko bei ya juu ya minada yote katika msimu mzima uliopita, ndio maana sisi wakulima tumeendelea kuzipokea bei hizi kwa sababu kwetu bado zina maslahi makubwa" ameeleza mkulima huyo.


Aidha kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa RUNALI Ndugu Shaban Yusuph Kupela, amewaeleza wakulima kuwa bei ya korosho inaamuliwa na hali ilivyo sokoni na wafanyabishara ndio wanaoleta bei kulingana na mahitaji yao kwa wakati huo.


"Sisi kazi yetu ni kupeleka Korosho sokoni, wenzetu TMX wanasimamia mfumo wa uendeshaji wa minada kimtandao na kuwaunganisha wakulima na wanunuzi, na mnunuzi anayeweka bei ya kuridhisha anauziwa mzigo, huo ndio utaratibu na kama mnavyoona mwaka huu wote tunashuhudia kwa pamoja mfumo wa kisasa wa uendeshaji wa minada na faida zake" amesema Kupela.

No comments: