Na Epifania Magingo,Manyara
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga amewaasa wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kupiga kura ya kuchagua Viongozi wa Serikali zà Mtaa huku akiwataka kutokaa kwenye vituo hivyo mara baada ya kupiga kura.
Sendiga ameyasema hayo Leo 27 November wakati alipojitikeza katika kupiga kura kwenye Kituo cha kwaraa Wilayani Babati Mkoani Manyara na kusema kuwa suala la kupiga kula ni Haki ya Kila Mtanzania.
"Na hatutegemea kwakweli kuona watu wameendelea kukaa kwenye vituo vya kupigia kura baada ya kupiga kura,watakaobaki labda wanashindwa zao binafsi lakini wanapaswa kwenda nyumbani na kusubiria matokeo yatakapotangazwa ,na Mimi nimeshapiga Kura nimetimiza wajibu wangu wa kikatiba tayari".amesema Sendiga
Amesema,zoezi Hilo katika Kituo cha kwaraa linaendelea vizuri na usalama upo wa kutosha hivyo wananchi ambao Bado wako majumbani wajitokeze Kwa wingi kwenda kupiga kura ambao wamejiandikisha katika Kituo hicho.
Amesema,Uchaguzi utakua wa haki Kwa kuzingatia Demokrasia na hivyo na alieshinda ndio atakaetangazwa.
Nao baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kupiga kura wamesema zoezi Hilo linakwenda vizuri na ni jambo la kihistoria ambalo litasaidia kuleta maendeleo ndani ya Mitaa.
"Mimi nimeshapiga Kura na Serikali imefanya kazi kubwa sana imeonesha ukomavu wa kidemokrasia na imetoa Elimu kubwa sana,kwaio niwaombe wenzetu waliopo majumbani wajitokeze kuja kupiga kura".amesema Eliakim Paulo
Ikumbukwe kuwa Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali zà Mtaa hufanyika Kila baada ya miaka 5 na Kila Mtanzania anahaki ya kikatiba kupiga kura ya kuchagua kiongozi à nayemtaka.
No comments:
Post a Comment