Shirika la Habitat lawajengea Nyumba familia maskini Manyara - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 15 November 2024

Shirika la Habitat lawajengea Nyumba familia maskini Manyara

 



Na Epifania Magingo,Manyara 


maipacarusha20@gmail.com


Kaya  8 Wilayani Hanang' Mkoani Manyara zimenufaika kwa kujengewa nyumba za kisasa za Kuishi zenye thamani ya Shilingi milioni 16 na laki 2 Kwa Kila Moja na Shirika lisilo la Kiserikali Tanzania (Habitat for Humanity Tanzania) kwa Kushrikiana na Serikali ya Tanzania.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi wa wanufaika wa nyumba hizo wameeleza kuwa hapo awali walikuwa wakiishi katika mazingira magumu kabla ya kujengewa nyumba hizo na kuishukuru Serikali kwa kuruhusu mashirika binafsi kuja kufanya kazi hapa Nchini.


"Nilikua nakaa na nyumba ambayo ni ndogo chumba kimoja na sebule  ilikua haitoshi kwa familia nina watoto tisa, na sasa nimejengewa nyumba nzuri yenye ubora na choo Cha kisasa nashukuru sana na Sasa nitalala vizuri, naomba Shirika hili na Serikali wasaidie wengine wenye shida kama Mimi".  Magdalena Burra amesema


"Kwakweli maisha yalikua magumu sana tulikua tunajibana kulala wajukuu nalala nao chumbani na mbuzi wanalala sebuleni hapo nilipokua napikia,na usipokua na nyumba nzuri binadamu huezi kuheshimika, Ninashukuru Shirika la Habitat kwa kutujengea nyumba,ninafuraha isio na mwisho, Ninashukuru Serikali kwa kuleta Hawa watu, mashirika mengine wajitokeze kujengea wengine". Whiteness Kunguda amesema


Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali Tanzania (Habitat for Humanity Tanzania) Magdalena George amesema Shirika lilikua na bajeti ya Shilingi milioni 195 ambapo fedha hizo zilienda katika mgawanyo wa kujenga nyumba 8 zenye thamani ya Shilingi milioni 16 na laki 2 Kwa Kila Moja huku fedha nyingine zimetumika Kwa kufanyia mafunzo kwa Vijana  21 kujifunza namna ya ujenzi wa nyumba bora kwa gharama nafuu.


"Hao vijana 21 tumefanya nao mafunzo ya ujenzi wa gharama nafuu kwamba unawezaje kujenga nyumba ya gharama nafuu na inakua bora lakini pia tunawapeleka veta tunataka wakapate ile Elimu ya kitaalamu kabisa ya ujenzi ili wapate vyeti na mbeleni itawasaidia kupata ajira kwenye makampuni ya ujenzi na kujiajiri wenyewe"Magdalena George amesema 


Aidha,amesema Shikirika hilo linafanya kazi kwa ukaribu na Serikali na kwamba wameguswa kwa kutoa msaada kwa kuwajengea nyumba hizo ili kusitiri utu wa mtu kwakua hapo awali chumba kimoja walikua wakiishi watu wengi.


"Shirika letu linaangalia Kaya masikini zisizoweza kujenga nyumba,kazi ambayo inafanya ni kubadilisha maisha ya watu,Mimi pia nimejisikia faraja kwa kukamilisha ujenzi huo,kwaio wamama kama hao waliojengewa nyumba wanaona tumaini jipya katika maisha".Magdalena George amesema


Katibu Tawala wa Wilaya ya Hanang' Athuman Likeyekeye ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Wilaya amekata utepe wa ufunguzi wa nyumba hizo na kulipongeza Shirika la Habitat for Humanity Kwa kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuwajengea nyumba hizo kaya masikini.


"Nyinyi Habitat mnaunga mkono pale ambapo Dakitari Samia Suluhu Hassan Rais wetu makubwa ambayo ametufanyia wanahanang' na Watanzania kwa ujumla kwaio Mimi kwa niaba ya Mkuu wetu wa Wilaya nimezipokea nyumba hizi,na nisema shukrani sana na wanufaika wa nyumba hizo wakazitumie kwa furaha na amani".

No comments: