Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara Bahati Stafu Haule akizungumza na waandishi wa habari |
Na Epifania Magingo, Manyara
maipacarusha20@gmail.com
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Mkoa wa Manyara (TAKUKURU) imetoa tamko kuelekea Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali zà Mtaa kwamba hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya yeyote atakaebainika kutoa na kupokea Rushwa katika nyakati hizo kwakuwa Rushwa ni uhujumu Uchumi.
Kwa mujibu wa ibara ya (4) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na kwamba ibara ya (9)inasema Moja kati ya jukumu kubwa la Serikali ni kuondoa Rushwa Nchini huku ibara ya (8)inasema Serikali itapata Madara kutoka kwa wananchi na itawajibika kwa wananchi.
Hayo yamezungumzwa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara Bahati Stafu Haule wakati akitoa taarifa ya tathimini ya utendaji kazi wa Taasisi hiyo kuanzia Julai Hadi September ambapo amesema lengo kuu ya ibara hiyo ni kuimarisha demokrasia na wananchi wajue kwamba wanatakiwa kutumia demokrasia hiyo kuharikisha maendeleo ya Taifa.
"Tunakemea Rushwa kwenye Uchaguzi kwasababu Rushwa ni kosa la jinai, lakini pia Rushwa ni kosa la kiimani,maandiko matakatifu kwenye vitabu vyote vya Dini vinakataza Rushwa,lakini pia ni kosa Kwa mujibu wa utumishi wa umma,ni kosaa kimaadili,kwaio Rushwa ni adui wa haki na maendeleo".
Aidha,TAKUKURU pia katika utendaji kazi wake imeweza kuokoa kiasi Cha Shilingi milioni 13 na laki nane,sabuni na tisa elfu mia tatu kumi na Tano(13,879,315) ambapo kiasi Cha Shilingi 4,840,000 kilitokana na thamani ya dawa zilizokuwa zimeibiwa kwenye Zahanati ya Orkirung'rung na kurejeshwa baada ya kufanyika ufuatiliaji wa kero hiyo iliyoibuliwa kupitia kikao Cha TAKUKURU rafiki kilichofanyika Wilaya ya Simanjiro.
Hata hivyo, mpango wa TAKUKURU Mkoa wa Manyara 2022/23 Hadi 2025/26 itaimarisha juhudi za kuzuia vitendo vya Rushwa kwa kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuhamasisha ushiriki wa wananchi katika kuzuia Rushwa kupitia nyezo mbalimbali za uelimishaji ikiwemo klabu za wapinga Rushwa mashuleni na vyuoni.
No comments:
Post a Comment