TAKUKURU MOROGORO YABAINISHA SEKTA ZINAZOLALAMIKIWA KWA WINGI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 26 November 2024

TAKUKURU MOROGORO YABAINISHA SEKTA ZINAZOLALAMIKIWA KWA WINGI

 

Na Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


TAASISI ya Kuzuaia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Mkoa wa Morogoro imebainisha Sekta zilizolalamikiwa ambapo Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) imeingoza kwa malalamiko ikifatiwa na sekata ya Maji na Ardhi.


Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Morogoro Pilly Mwakasege alieleza hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.


Mwakasege alisema Tamiseni malalamiko mengi ni kwa watendaji wa vijiji,mitaa na kata wapatao 32, Sekta ya Maji wakiwa 11 na Ardhi 10 na alitaja maeneo mengine yanayolalamikiwa kuwa ni pamoja na sekta ya Elimu 6,Afya 6,taasisi ya fedha 6, Polisi 6 na Wakala wa Barabara mijini na vijijini TARURA yakiwa malalamiko 5.


Mkuu huyo wa Takukuru alisema maeneo mengine yenye malalamiko ni ujenzi,mifugono,nishati, Kilimo,Mahakama, Tasaf,Vyama vya Ushirika, Maliasili, Vyama vya siasa, Baraza la Ardhi.


"Mpaka sasa kesi mpya ni 15 na zinazoendelea ni 26 lakini kesi zilizoshinda ni 9, zilizoamuliwa 15 na zilizoondolewa mahakamani ni kesi 4,"alisema.


Aidha mkuu huyo wa Takukuru alisema Taasisi hiyo imefanikiwa kutoka kiasi cha sh 27 milioni kwa Jamson computer service and Stationary iliyopata zabuni na kushindwa kuwasilisha vifaa vya TEHAMA vilivyokusudiwa  kusambazwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.


"Baada ya TAKUKURU kumtaka mzabuni kuwasilisha vifaa hivyo ili viweze kitumika kwa malengo yaliyokusudiwa mzabuni amefanikiwa kuwasilisha vifaa vya thamani ya sh milioni 5.9 kukabidhi kwa Mkurugenzi na vifaa vilivyosalia nI vya thamani ya sh milioni 21.1. 


Mwakasege aliwataka wazabuni kutekeleza wajibu wao kama walivyoingia mikataba ya kutoa huduma ipasavyo na kwamba Takukuru haitasita kuwachukulia hatua za kisheria ukiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani wale wenye mienendo ya ubadhirifu na kujinufaisha na fedha za Serikali.


Pia Takukuru imefanya ufatiliaji utekelezaji wa miradi ya maendeleo 24 kwenye Sekta za Elimu, Maji, Barabara na Afya iliyopo katika hatua mbalimbali za utekelezaji yenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 7.23 ambayo mapungugu kadhaa yalibainika na kupendekeza hatua za kuchukuliwa.


Takukuru mkoa imeendelea kutoa elimu kwa umma kwa kufanya mikutano 66,semina 103, uimarishaji wa Klabu za wapinga Rushwa kwenye shule za msingi,sekondari na vyuo 115.


Johannes Solomon mkazi wa Manispaa ya Morogoro akizungumza na Mwandishi wa Habari hii alisema ni vyema Takukuru ikaendelea kutoa elimu kwa wananchi kwani inasaidia kupata kufahamu zaidi kwao.


Solomoni alisema suala la Rushwa hasa kwenye maeneo ya vijijini na  mitaa bado ni tatizo kutokana na baadhi ya watendaji kuomba Rushwa bila woga.


Mwisho.

No comments: