AMUUA MKE KWA KUMPIGA NA FIMBO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 4 December 2024

AMUUA MKE KWA KUMPIGA NA FIMBO




Mwandishi wetu ,MAIPAC KIBAHA

maipacarusha20@gmail.com


JESHI la polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Godfrey Killu (30) mkazi wa Mbwate kata ya Mkuza Wilaya ya Kibaha kwa tuhuma za mauaji ya aliyekuwa mke wake Elizabeth Sindikila (26).

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mjini Kibaha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Salim Morcase amesema tukio hilo lilitokea Desemba Mosi wakati Godfrey alipoenda na Elizabeth kunywa pombe za kienyeji na ulipofika muda wa kuondoka nyumbani ndipo walipoanza kugombana.

Kamanda Morcase amesema Elizabeth alipotakiwa kurud nyumbani aligoma na kusababisha ugomvi ambao Godfrey alilazimima kutumia fimbo kumpigia Ili waelekee nyumbani.

"Baada ya kumpiga kwa kutumia fimbo maeneo mbalimbali ya mwili na kuona hali ya mke wake sio nzuri alilazimika kumpeleka Hospitali ya Rufaa ya Tumbi kwa matibabu na baada ya muda ilithibitika amefariki," amesema.


Amesema Elizabeth alifariki akiwa anapatiwa matibabu kutokana na majerqha aliyopafa katika maeneo mbalimbali ya mwili.

Kamanda Morcase amesema baada ya mahijiano na mtuhumiwa alikiri kuhusika na kifo cha mke wake kwa kumpigia na fimbo .


Amesema mtuhumiwa anatarajia kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.


Mwisho

No comments: