DCEA YATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU (CWT) MKOA WA ARUSHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 31 January 2025

DCEA YATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA CHAMA CHA WALIMU (CWT) MKOA WA ARUSHA

 




Na Prisca Libaga Arusha


maipacarusha20@gmail.com 


Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini tarehe 30.01.2025 imetoa elimu juu ya mbinu za kuwaepusha wanafunzi na tatizo la dawa za kulevya kwa viongozi 58 wa matawi ya Chama cha Walimu (CWT) Mkoa wa Arusha katika Ukumbi wa Ofisi za Chama hiko jijini Arusha. 


Walimu Viongozi hao walifundishwa uhusiano wa tatizo la dawa za kulevya na changamoto za afya ya akili, kuwa matumizi ya dawa za kulevya kwa wanafunzi inaweza kupelekea kupata magonjwa ya akili na kufeli darasani. 


Pia walihamasishwa kushirikiana na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa hizo kupitia namba ya simu ya bure ya 119.


MWISHO

No comments: