KAGANDA AWASIHI WANAFUNZI KUDUMISHA NIDHAMU NA KUSOMA KWA BIDII - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 15 January 2025

KAGANDA AWASIHI WANAFUNZI KUDUMISHA NIDHAMU NA KUSOMA KWA BIDII

 







Na Epifania Magingo,Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 



Katika utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daktari Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Mtatifikolo Kaganda, amefanya ziara ya kutembelea shule mbalimbali za Msingi na Sekondari katika Wilaya hiyo ikiwa ni siku ya ufunguzi wa mwaka wa masomo 2025.  


Katika ziara hiyo, Kaganda ametoa wito kwa walimu, wazazi na walezi kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanahudhuria masomo kwa wakati pasipo visingizio vyovyote na kusisitiza kuwa Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inaweka  mazingira bora ya elimu kwa wanafunzi wote


Aidha, Kaganda amewasihi wanafunzi kusoma kwa bidii, kuheshimu walimu na kudumisha nidhamu katika kipindi chote cha masomo.


Pia, amewataka walimu kuendelea kusimamia malezi bora ya Kiafrika kwa wanafunzi ili kulinda na kuendeleza utamaduni wa Taifa. 


"Elimu ni silaha muhimu kwa maendeleo, Hakikisheni mnaipata kwa bidii na nidhamu ili kuifikia ndoto yenu," Alisema 


Kwa upande wao, wanafunzi walimshukuru  Kaganda na kuwasilisha salamu za shukrani kwa Serikali kwa jitihada kubwa za kuboresha elimu huku  wakiahidi kusoma kwa bidii na kufikia malengo yao ya kitaaluma.  


Ziara hii ni sehemu ya dhamira ya Serikali kuhakikisha elimu bora inatolewa kwa watoto wote wa Tanzania, huku ikizingatia maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuboresha mazingira ya shule na kuhamasisha ushirikiano wa jamii katika kukuza elimu.

No comments: