MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAENDELEA MASASI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 31 January 2025

MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAENDELEA MASASI

 



Na Mwandishi Wetu Maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Timu ya Mama Samia Legal Aid Campaign imeendelea kukutana na wananchi na kutoa elimu na ushauri wa kisheria kwa wananchi wa Halmashauri ya Masasi Mkoani Mtwara.


Leo Januari 30,2025 Kampeni hiyo imeyafikia makundi mbalimbali wakiwepo wanafunzi, ambapo moja ya  shule zilizotembelewa leo ni  Chikunja Sekondani ambayo wanafunzi wake wamepata fursa ya kupata elimu ya masuala mbalimbali ya kisheria.


Wanafunzi hao pia wamekumbushwa juu ya masuala ya ukatili wa kijinsia na wajibu wao wa kusoma kwa bidii ili watimize ndoto zao, lakini vilevile kutoa taarifa pale wanapokutana na viashiria vya uvunjifu wa sheria katika jamii.


Mratibu wa Kampeni hiyo katika Halmashauri ya Masasi Ndg. Amani Kilua ameeleza kuwa kumeendelea kuwepo na muitikio kutoka kwa wananchi, ambao wengi wao wamekuwa wakiwasilisha changamoto mbalimbali za kisheria kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi na ushauri.


" Leo Januari 30, 2015 tumewafikia wananchi katika vijiji vilivyopo Kata za Chikunja na Nanditi kwa ajili ya kuwahudumia, kila mahali tulipopita wananchi wameonesha uhitaji wa kupatiwa huduma na kufurahia huduma hii kuwafikia katika maeneo yao jambo ambalo limewaondolea usumbufu na gharama" ameeleza Kilua


Kampeni ya Mama Samia Legal Aid katika Mkoa wa Mtwara ilizinduliwa Januari 24,2025 na Mkuu wa Mkoa huo Kanali Patrick Sawala, ambaye aliwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika Halmashauri zao kwa ajili ya kupata msaa wa Kisheria.

No comments: