MEYA WA JIJI LA ARUSHA AZINDUA MITAMBO YA UKARABATI WA BARABARA YENYE THAMANI YA BILIONI 1.7 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 28 January 2025

MEYA WA JIJI LA ARUSHA AZINDUA MITAMBO YA UKARABATI WA BARABARA YENYE THAMANI YA BILIONI 1.7






 Na Pamela Mollel Arusha 


maipacarusha20@gmail.com 


Mstahiki Meya Jiji la Arusha Mhe Maxmillian Matle Iranqhe amezindua mitambo Mipya ya ujenzi na ukarabati wa barabara za ndani zilizo chini ya Usimamizi wa Jiji la Arusha zilizogharimu bilioni 1.7


Aidha barabara hizo ni mbazo zipo chini ya TARURA kwa lengo la kuhakikisha barabara za ndani zina kiwango kizuri kwa wananchi kutumia katika shughuli zao za kila siku


Katika hafla hyo Mitambo iliyozinduliwa ni pamoja na mtambo wa  greda moja na malori makubwa mawili


Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Arusha Meya Maxmillian, anawakumbusha watendaji kuhakikisha wanatunza mitambo hiyo ili iweze kufikia Malengo kusudiwa


Pia aliwataka Waheshimiwa Madiwani wa Jiji la Arusha kuhakikisha wanahamasisha wananchi kushiriki shughuli za usafi wa mitaa ili Wageni wanaotembelea jiji la Arusha wavutiwe zaidi 


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha John Kayombo amepongeza hatua hiyo ya upatikanaji wa mitambo hiyo ambayo inakwenda kutatua changamoto katika barabara za ndani wanazotumia wananchi


Aliongeza kuwa moja ya changamoto walizokutana nazo Madiwani wake ni pamoja na kuburuzwa katika tope kutokana na ubovu wa barabara ambapo amekiri hali hiyo kutojitokeza tena.


Mwisho

No comments: