WANANCHI NANYAMBA TC WAFURAHISHWA NA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA WA MAMA SAMIA LEGAL AID. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 28 January 2025

WANANCHI NANYAMBA TC WAFURAHISHWA NA HUDUMA YA MSAADA WA KISHERIA WA MAMA SAMIA LEGAL AID.

 




Na Mwandishi Wetu Maipac 


maipacarusha20@gmail.com


Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ijulikanayo kama Samia Legal Aid, imeendelea kuwafikia wananchi katika Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Mtwara.


Katika Halmashauri ya Mji Nanyamba Mkoani Mtwara, leo tarehe 27/1/2025 wananchi wameendelea kupata huduma baada ya watendaji wa Kampeni hiyo kufika katika vijiji vya Malongo, Majengo na Njengwa.


Wakizungumza na vyombo vya habari wananchi hao wameeleza kufurahiswa na huduma hiyo ya msaada wa kisheria inayoambatana na elemu, wakisema kuwa imewasaidia kujua haki zao na masuala mengine ya kisheria yaliyokuwa yakiwasumbua kwa muda mrefu.


Aidha Wananchi hao walimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.samia kwa ubunifu huo ambao wamesema umewafikia kwa wakati muafaka ambao wana haja ya kuzifahamu haki zao za kisheria.


 "Kampeni hii ni muhimunsana, na vitu kama hivi vingekuja mapema tusingekuwa na migogoro ikiwemo ya ardhi,ndoa,mirathi na dhuluma zingine wanazofanyiwa wananchi" ameeleza Hassan Dadi mkazi wa Kijiji cha Malongo Nanyanba TC.


Mratibu wa kampeni hiyo katika Halmashauri ya Nanyamba Ndg. Christopher kabado Kabado amewataka wananchi kuendelea kujitokeza na kupata huduma ambazo ameeleza kuwa zinatolewa bure na inaratibiwa na Wizara ya katiba na Sheria.

No comments: