MWENYEKITI MIRERANI ATANGAZA WAJUMBE WA KAMATI ZAKE - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 11 January 2025

MWENYEKITI MIRERANI ATANGAZA WAJUMBE WA KAMATI ZAKE

 



Na Mwandishi wetu, Mirerani


maipacarusha20@gmail.com 


MWENYEKITI wa Mamlaka ya Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Hans Nkya ametangaza majina ya wajumbe wa kamati tatu zinazounda mamlaka hiyo.

 

Akizungumza kwenye kikao cha kwanza cha mamlaka hiyo baada ya uchaguzi, Mwenyekiti huyo amesema kamati hizo zitadumu madarakani kwa muda wa mwaka mmoja wa 2025/2026.


Nkya amesema kamati ya kudhibiti Ukimwi  itaongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Mamlaka hiyo Prim Barnabas na wajumbe ni David Makala, Claudia Dengez, Omary Konki na Jacklen Momo.


Amewataja wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Abraham Mmary, Yotham Lolo, Gadi Msuya, Anthon Musiba, Kweka na Diwani wa kata ya Naisinyai Taiko Kurian Laizer.


Amewataja wajumbe wa kamati ya Elimu, Afya na Maendeleo ya Jamii ambayo Mwenyekiti wake Eliakana Mkumbo ni Omary Hussein, Christopher Chengula, Sifa Lilama, Juma Seleman.


Amewataja wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Johari Mwaselela, Twaha Mpanda, Andrew Nyambo, Happy Msuya, Abutway Ramadhan na Diwani kata ya Endiamtu Lucas Zacharia.


Amewataja wajumbe wa kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira, inayoongozwa na Mwenyekiti Idd Abdi ni Hamad Malya, Songelael Nalogwa, Sofia Kisesa na Jema Lilama.  


“Wajumbe wengine ni Habiba Omary, Amiry Jamhuri, Okwaro Ochieng’, Okinyi Marire, Adam Kobelo, Mweta Omary na Diwani kata ya Mirerani Salome Mnyawi,” amesema Nkya.


Hata hivyo, Nkya amesema kwa ridhaa aliyopewa amewateua wajumbe wawili kwenye kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ambao ni Jema Lilama na Omary Hussein (Ombopa). 


MWISHO

No comments: