WAKAZI 1,500 WA IBULA WANUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 11 January 2025

WAKAZI 1,500 WA IBULA WANUFAIKA NA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA

 





Na Mwandishi wetu Rungwe .


maipacarusha20@gmail.com


Wakazi zaidi ya 1500 wa eneo la katago kijiji cha Ibula kitongoji cha Kibumbe wamenufaika na huduma ya maji ya Bomba baada ya Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF kuwajengea mradi wa kisima cha maji safi na salama kilichoboreshwa kwenye chanzo cha maji cha Mto ambapo wameomba waruhusiwe kuvuta maji kwenye nyumba zao.


Akizungumza na mwandishi wa habari hii, kwenye eneo ulipojengwa mradi huo, Ntuli Fungo mkazi wa kijiji cha Ibula wameushukuru uongozi wa TASAF kwa kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji safi na salama ambapo amewaomba waruhusu wananchi kuvuta maji kwenye nyumba zao.


"Maji haya ni salama, tunayatumia na hatuzuliki kama unavyoyaona ni masafi sana ila tu tunaomba turuhusiwe kuvuta hadi majumbani mwetu ili uwe rahisi zaidi kutumia kwenye shughuli za nyumbani na hata bustani".Alisema Ntuli.


Nae Raphael Mwampamba mkazi wa Ibula amesema bado kijiji hicho hakijapata huduma ya maji ya bomba hivyo miradi ya kisima cha maji kilichojengwa na Tasaf kimesaidia kutatua kero ya maji kijijini hapo nyakati za kiangazi ambapo wananchi wanauhakika wa kupata huduma hiyo.


"Ninaupongeza uongozi wa Tasaf makao mkuu kwa kutoa pesa ya kuboresha hiki kisima kwani wamesaidia kutuondolea kero kubwa ya upatikanaji wa maji kwenye kijiji hiki,pia tumeweza pata ajira za muda nakusaidia kupata kupata cha kuendesha familia zetu," Alisema


Mwezeshaji toka TASAF Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Robert Mwakilambo amesema, mradi huo ulibuniwa na walengwa wenyewe kupitia mradi wa PWP baada ya wanufaika kuona changamoto na kuigeuza kuwa fursa .


Amesema, mradi huo umekua Mkombozi kwa wananchi wa kijiji hicho kwani kiuhalisia mwanzo walikua hawana chanzo kingine cha maji na baada ya kujengewa na kuboresha kisima hicho wanachota maji bila matatizo. 


"Kiuhalisia ni msaada mkubwa kwao mwanzo walikua hawana kisima wanatumia bakuri na ndoo kuchota maji hivyo walitumia maji ambayo si salama ila sasa usalama wa maji umehimalika baada ya kisima kuboreshwa" Alisema 


Kwa upande wake ofisa ufatiliaji TASAF Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Yesaya Mwaluhisi amewataka wananchi kulinda na kutunza miradi ya miundo mbinu ya maji ambayo imetekelezwa na TASAF kwenye vijiji vyao kwani miradi hiyo ni yao na siyo ya serikali kwakua inawanufaisha wao hivyo waitunze ili iwasaidie wao na vizazi vijavyo kama ambavyo TASAF I,ilivyowasaidia kupanda miti ya asili inayotunza mazingira kwenye vyanzo vya maji.


Mwisho

No comments: