SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAENDELEA WILAYANI NEWALA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 29 January 2025

SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN YAENDELEA WILAYANI NEWALA

 





Na Mwandishi Wetu Maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Wananchi katika Halmashauri ya Newala Mji Mkoani Mtwara, wameendelea kufikiwa na watendaji wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia na kupata fursa ya kupata elimu juu ya masuala mbalimbali ya kisheria.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti leo Tarehe 29 Januari2025, wananchi wa Vijiji vya Kilidu, Mkulungulu na Magombo kata ya Mkulungulu wameeleza kunufaika na kampeni hiyo kutokana na elimu ambayo wameipata.


"Hii ni kampeni ambayo imekuja kwa wakati wake, sisi wananchi tunamshukuru Mama Samia kwa msaada huu ambao unatupa nafasi ya kutatuliwa changamoto zetu zinazotukubali bila kusafiri na kutumia gharama kubwa" ameeleza Amina Ausi mkaazi wa Kilidu.


Aidha kwa upande wake Mratibu wa Kampeni hiyo Wilaya ya Newala Doreen Mhina amewasisitiza wananchi kujitokeza katika maeneo mbalimbali yanayofikiwa na huduma hiyo, ili waweze kuwasilisha changamoto zao na kutafutiwa ufumbuzi.


Amesema wameendelea kuwafikia Wananchi na kuwasikiliza sambamba na kutoa elimu ya masuala mbalimbali yakiwepo ya ukatili wa kijinsia, Mirathi na migogoro ya ardhi.

No comments: