Shirikisho la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) laanzishwa kutetea haki za wanahabari. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 17 January 2025

Shirikisho la Waandishi wa habari Afrika Mashariki(FEAJ) laanzishwa kutetea haki za wanahabari.

 




Baadhi ya Viongozi wanaounda shirikisho hilo




Na: Mwandishi wetu,Kigali


maipacarusha20@gmail.com 


Shirikisho jipya la Waandishi wa habari Afrika Mashariki (FEAJ) limeanzishwa ili kusaidia kutetea haki na maslahi ya  wafanyakazi katika vyombo vya Habari Afrika Mashariki na kuchaguwa viongozi wapya..


Shirikisho hilo limeanzishwa na viongozi wa vyama vya vya wafanyakazi katika vyombo vya  habari Afrika ya Mashariki katika mkutano uliofanyika Kigali nchini Rwanda.


Katika mkutano huo ambao ulisimamiwa na shirikisho la waandishi wa habari barani Afrika (FAJ), mwanahabari Erick Oduor kutoka nchini Kenya alichaguliwa kuwa Rais wa shirikisho hilo.


Odour ni Katibu wa chama cha umoja waandishi wa habari nchini Kenya (KUJ)


Wengine waliochaguliwa ni Patrick Oyet  makamu mwenyekiti kutoka nchini Sudani na Solange Ayanone kutoka Rwanda akichaguliwa kuwa Katibu Mtendaji na mweka hazina.


Wengine waliochaguliwa ni kuunda kamati ya utendaji ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi katika vyombo vya habari Tanzania (JOWUTA) Mussa Juma na Promise Twinamukye kutoka Uganda.


Viongozi hao kwa mujibu wa katiba ya FEAJ watakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka  mitatu.


Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Oduor aliahidi shirikisho hilo kufanyakazi ya kuwaunganisha wanahabari katika masuala ya kutetea haki zao na masuala ya kitaaluma.


Katika mkutano huo, viongozi wa shirikisho hilo walikubaliana makao makuu yatakuwa Nairobi nchini Kenya. 


Nchi ambazo zinaunda shirikisho hilo ni Kenya, Somalia, Rwanda, Tanzania, Burundi, Uganda, South Sudan, Sudan, Ethiopia, Djibouti, Seychelles and Comoros.


Awali Rais wa FAJ,Omar Faruk akizungumza katika mkutano huo, alisema shirikisho hilo ni utekelezwaji wa matakwa ya FAJ.


Alisema tayari kanda nyingine barani Afrika zimeunda mashirikisho yao na yanafanya kazi nzuri kuwaunganisha wanahabari.


Uchaguzi huo wa FEAJ uliambatana na mafunzo ya wanahabari barani Afrika kuhusiana na masuala ya wahamiaji wanaotafuta kazi (Labour Migration).


Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na shirika la kazi duniani (ILO) Kwa kishirikiana na FAJ na Chama cha waandishi habari Rwanda(ARJ) .


Mwisho



No comments: