Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi Balozi Ombeni Sefue akizungumza na wadau wa Kodi Mkoani Manyara |
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen SENDIGA akizungumza na wadau wa Kodi Mkoani Manyara |
Wafanyabiashara na wadau wa Kodi wakimsikiliza Balozi Ombeni Sefue |
Na Epifania Magingo, Manyara
maipacarusha20@gmail.com
Wadau wa Kodi Mkoani Manyara wameiomba Serikali kuboresha mifumo ya Kodi ambayo ni kandamizi kwakua inarudisha Maendeleo ya Uwekezaji kwenye Sekta ambazo zinahitaji kulipa Kodi kwa hiyari ili kukuza Pato la Taifa.
Hayo yamezungumzwa katika kikao Cha Tume ya Rais ya maboresho ya Kodi na wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa Kodi wa Mkoa wa Manyara kwenye ukumbi wa Mkutano wa Ofis ya Mkuu wa Mkoa.
Julian Khambayta ambaye ni Katibu Mtendaji wa Manyara Sunflower Oil Prosesor Association (MASUPA) mmoja wa washiriki kwenye kikao hicho ameishauri Serikali kufanya maboresho ya mifumo ya Kodi ili iweze kusomana ili iwe rahisi wafanyabiashara kulipa Kodi kwa wakati.
"Muheshimiwa Mwenyekiti risiva za TRA ni changamoto sana, mifumo haisomani, mtu wa IT anatakiwa aangalie kwa macho makubwa, mifumo ni mizuri lakini iboreshwe ili isomane". Kambaita amesema
Zainabu Sadiki ambaye ni Katibu Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara Viwanda na Kilimo TCCIA Mkoa wa Manyara amesema kumekuwa na utitiri wa ulipaji Kodi kwa wafanyabiashara ambao unakua kikwazo na kuiomba Serikali kuweka mfumo rafiki ambao utasaidia ulipaji wa Kodi kwa urahusi.
"Changamoto Moja wapo ni mapitio ya Kodi kumekua na utitiri mwingi wa kodi pamoja na tozo, utakuta mfanyabiashara mmoja analipa vitu vingi kwa wakati mmoja utakuta kuna VAT, na maelekezo mengine mengi ya masuala ya TBS". Alisema
Wakati wa Kikao hicho, Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Maboresho ya Kodi Balozi Ombeni Sefue amesema lengo la kupokea maoni, kero, changamoto na mapendekezo kutoka kwa wananchi ni namna Bora ya Serikali irahisishe kuanzisha bishashara, baishara kukua na kulipa Kodi huku akiahidi maoni kufikisha kwa Muheshimiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan.
" Tungeweza kusema wataalamu wa kutosha wenye masuala ya Kodi tukakaa tukajifungia tukaandaa mapendekezo yetu na kupeleka Kwa muheshimiwa Rais lakini tunakua hivyo sio alivokusudia muheshimiwa Rais, mapendekezo ambayo tutarejesha kwake ni muhimu yakaakisi mapendekezo ya wananchi ". Sefue amesema
Balozi Sefue amesema maeneo ya Wafanyabiashara yaliyotembelewa na Tume imebainika kuwa hakuna mfanyabiashara aliekataa kulipa Kodi basi walitoa maoni kuwa mazingira ya ulipaji Kodi yamekua magumu.
Kwa Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga ameipongeza tume hiyo kwa kukusanya kero na maoni yenye lengo la kuboresha bishashara na ukusanyaji wa Kodi rafiki kwa watanzania wote.
" Ili tupate maendeleo, uchumi uweze kukua, tunahitaji Kodi, ambapo ili kuweza kukusanya Kodi vizuri tunahitaji kuangalia kero zilizopo ziweze kufanyiwa kazi ndo lengo kuu la Tume hivyo tutoe ushirikiano". Sendiga amesema
No comments:
Post a Comment