VIONGOZI MANYARA WATAKIWA KUHESHIMU MAAMUZI YA MAHAKAMA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 4 February 2025

VIONGOZI MANYARA WATAKIWA KUHESHIMU MAAMUZI YA MAHAKAMA

 





Na Epifania Magingo, Manyara 


maipacarusha20@gmail.com 


Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Cuthbert Sendiga  alishiriki katika kilele cha madhimisho ya siku ya Sheria kwa mwaka 2025 Mkoa wa Manyara akiwa Mgeni Maalumu na Mgeni Rasmi ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Kanda ya Manyara Mheshimiwa John Kahyoza. 


Akitoa salamu wakati wa maadhimisho hayo 3 Februari 2025 Mkuu wa Mkoa alieleza kuwa kwa kuzingatia Ibara ya 107A ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Viongozi wa Mkoa wa Manyara wataendelea kuheshimu na kutekeleza maamuzi yanayokuwa yametolewa na Mahakama.


Aidha,Sendiga amewataka wananchi wanaotafuta usaidizi wa kisheria kutumia Mawakili ambao wako rasmi badala ya Vishoka wa kisheria waliopo mtaani.


Nae ,Jaji Mfawidhi  Mheshimiwa John Kahyoza amempongeza Mkuu wa mkoa na wasaidizi wake kwa kuheshimu utawala wa Sheria na kutoingilia Maamuzi yanayoamuliwa Mahakamani.


Hata hivyo Jaji Kahyoza ametoa rai kwa Viongozi wa Dini na Mila kuelimisha Jamii kujiepusha na vitendo vya ukatili na ubakaji huku akisema kuwa  wahusika wa vitendo hivo wataishia gerezani pale itapothibitika.


Katika kuhitimisha hotuba yake Jaji Kahyoza alisisitiza kuwa Mahakama Kuu Kanda ya Manyara itajielekeza kiutendaji ili kwenda sambamba na malengo makuu ya dira ya Taifa ya maendeleo 2050.

No comments: