Wadau wa Sheria Tanga watoa ombi. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 4 February 2025

Wadau wa Sheria Tanga watoa ombi.







Na: Burhani Yakub,Tanga.


maipacarusha20@gmail.com 


Wadau wa sheria mkoani Tanga leo wameadhimisha kilele cha wiki ya sheria nchini huku wakiomba mahakama iongeze nguvu katika kuwasaidia washtakiwa ambao hawana mawakili.


Wakizungumza baada ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama.kuu Kanda ya Tanga, Katarina Mteule(pichani )kukagua gwaride na kuhutibia katika viwanja vya mahakama hiyo,wadau hao wamesema katika maboresho yanayofanyika ni vyema washtakiwa ambao hawana mawakili kusaidiwa.


Aisha Hassan ambaye ameeleza ushuhuda wake kwamba aliwahi kuhukumiwa kifungo katika mahakama ya Wilaya amwsema kukosa kwake kujua sheria kulisababisha atumikie kifungo.


"Nilipokuwa gerezani nilipata msaada wa wakili aliyejitolea kunikatia rufani akaendesha kesi nikaonekana sikuwa na hatia nikatoka gerezani....kule gerezani niliwaacha mahabusu wengi hawana mawakili"amesema Aisha


Mwenyekiti wa chama Cha wanasheria nchini TLS,Mkoa wa Tanga, Emmanuel Kiariro amesema chama hicho kimeongeza nguvu ya kutoa msaada wa kisheria kwa watuhumiwa wasio na mawakili ili kuhakikisha haki inatendeka.


"Tunaiomba mahakama iendelee kutupa washtakiwa ambao hawana mawakili Kwa kuwa TLS imejidhatiti kutoa huduma hiyo ya kisheria ili kesi ziweze kwenda Kwa Kasi"amesema Kiariro na kubainisha kuwa mkoa wa Tanga TLS ina wanachama 120 kati ya wanachama 12695.


Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu Kanda ya Tanga, Katarina Mteule amesema katika kipindi cha mwaka 2025 mahakama hiyo imejipanga kuendesha mashauri Kwa kasi ili kupunguza kesi zilizopo.


MWISHO

No comments: