Na Mwandishi Wetu, Arusha.
maipacarusha20@gmail.com
Tanzania yazindua rasmi mradi wa namna ya wafugaji na mifugo kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kuimarisha mazingira kupitia sekta za maji na malisho na pia kuboresha Uchumi kwa wafugaji.
Mradi huo unaofadhiliwa na jumuia ya ulaya kupitia shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa [FAO] kwa nchi saba za pembe ya Afrika mashariki ambapo kwa Tanzania utagharimu kiasi cha EUR milion 3.19 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 9.2.
Mradi huo utatekelezwa katika Wilaya mbili za Longido na Ngorongoro kwa kipindi cha miaka minne ambao utalenga maeneo manne ya upatikanaji wa maji ya uhakika ya mifugo kwa kipindi chote, upatikanaji wa malisho na mbegu bora za mifugo.
Akizindua mradi huo katibu mkuu wizara ya uvuvi na mifugo Prof.Riziki Shemdoe aliwataka maafisa mbalimbali wa serikali kutoka Wizara ya mifugo, Halmashauri na asasi za kiraia watakao simamia mradi huo kuhakikisha wanaandaa mpango kazi unaotekelezeka na kutoa matokeo yanayotarajiwa.
‘’Nimefurahi kuona makundi yote yamejumuishwa katika kuandaa na kusimamia mradi huu hivyo nawataka mnapokaa hapa kuandaa mpango kazi muandae mpango kazi kwa kuzingatia sheria za nchi na pia uwe ni wenye kutekelezekaa ili uweze kutoa matokeo Chanya na endelevu’’alisema Shemdoe.
Aidha katibu mkuu Shemdoe alisisitiza katika mpango huo matokeo ya mradi ni lazima yaonekane kwa macho sio katika makaratasi ambapo alisema kwa suala la maji lazima ihusishe utengenezaji wa malambo ya maji, majosho ya kuogeshea mofugo, masoko ya mifugo na mbegu bora ya mifugo ambazo zitanyanyua Uchumi wa wafugaji.
Akiongelea mradi huo Mtaalam wa mnyororo wa thamani kutoka [FAO] Dr. Moses Ole Neseli alisema mradi huo unaenda kukabiliana na makali ya mabadiliko ya tabia nchi ambapo licha ya Kwenda kuimarisha nyanda za malisho na maji lakini pia kuimarisha chanjo za mifugo katika maeneo mradi unapoenda kutekelezwa.
Ole Neseli alisema licha ya kusaidia katika maeneo hayo lakini pia mradi unalenga kuboresha Uchumi kwa jamii ya wafugaji ambao ndio wanahusika katika kuzalisha chakula kinachotokana namifugo.
Akiongea katika warsha hiyo ya uzinduzi wamradi Mkuu wa Wilaya ya Longido ambao ni miongoni mwa wanufaika wa Mradi huo [DC] Salumu kali alishukuru kwa Wilaya yake kuwa sehemu ya mradi huo kwani kwa miaka mingi wamekua wahanga wa mabadiliko ya tabia nchi.
Dc. Sali alisema kumekua na vifo vingi vya mifugo katika Wilaya yake nyakati za kiangazi kutokana na ukosefu wa maji na malisho ya uhakika na hivyo kupelekea wafugaji kupoteza mifugo mingi kwa sababu ya njaa.
Alisema anaamini mradi huo ukisimamiwa na kutekelezwa kama inavyokusudiwa basi wananchi wa Wilaya hiyo ambao kwa kiasi kikubwa ni wafugaji maisha yao yatabadilika na kunufaika na mazao yao ya mifugo.
‘’Ufugaji wa Longido ni biashara ni maisha na ndio Uchumi hivyo mradi huu unakuja kuongeza thamani ya biashara waliyonayo wakazi wa Longido ambapo itawafanya Uchumi wao kukua na hata kuongeza mapato ya Wilaya hiyo ‘’alisema DcSalum.
Mradi huo kwa nchi zote za pembe ya Afrika mashariki unatarajiwa kugharimu kiasi cha EUR milioni 47 kwa nchi zote saba ambapo mradi umepangwa katika kongani nne na Tanzania ikiwa kongani inayoihusisha na nchi ya kenya kupitia Wilaya za Kajiado na Narock upande wa Kenya na Longido na Ngorongoro kwa upande wa Tanzania.
==mwisho==
No comments:
Post a Comment