![]() |
Mkurugenzi wa Tanga Woman Gala, Nasoro Makau akizungumza na wanafunzi na wazazi wenye watoto wa mahitaji maalumu wa shule ya Msingi Maramba JKT Wilayani Mkinga |
![]() |
wanafunzi wa kitengo cha mahitaji maalumu shule ya Msingi Maramba JKT Wilayani Mkinga mara baada ya kutembelewa na wanachama wa Tanga Woman Gala wa jijini Tanga. |
Na: Burhani Yakub, Mkinga.
maipacarusha20@gmail.com
Kundi la wasichana wenye ulemavu limeelezwa kuwa linahitaji uangalizi na ulinzi wa karibu kutokana na kuwa katika hatari ya kubakwa pamoja na unyanyasaji mwingine wa kijinsia.
Mwenyekiti wa asasi ya Tanga Woman Gala,Latifa Makau ametoa angalizo hilo wakati wa ziara ya kuwatembelea wanafunzi wa kitengo cha mahitaji maalumu wa shule ya Msingi Maramba JKT Wilayani hapa
Amesema kutokana na kukabiliwa na changamoto za kimaumbile wasichana wenye ulemavu wanapokosa uangalizi wa karibu hutembea mitaani na kujikuta wakibakwa na wengine kufanyiwa ukatili mkubwa wa kijinsia.
"Lakini wengine walio ndani ya familia kwa sababu ya changamoto za kimaumbile iwe ni ya afya ya akili au viungo,wanafamilia huwabaka na kuwatisha wasiseme na kanakwamba si binadamu kama wengine"amesema Latifa.
Mwenyekiti huyo ameiomba jamii kushiri katika kuwalinda na kuwapa uangalizi wasichana wenye ulemavu ili waweze kuitimiza ndoto zao za maisha.
Mwenyekiti wa kitongojj cha Kwagatula Kijiji cha Maramba B Wilaya ya Mkinga ambako imejengwa shule hiyo, Johnson Haule amesema changamoto nyingine inayowakabili wanafunzi wa mahitaji maalumu shuleni hapo ni kutokuwepo kwa miundombinu rafiki ya vyoo hususani wasichana.
"Shuleni hapa tunao jumla ya wanafunzi 52 wenye mahitaji maalumu ambao wanaletwa asubuhi na kufuatwa jioni,kama tutajengewa Bweni tutakuwa nao muda mwingi itawasaidia wazazi wao kupata wasaa wa kufanya shughuli nyingine za kiuchumi"amesema Johnson
Mkurugenzi wa Tanga Gala,Nasoro Makau ameahidi kufikisha ngazi husika changamoto ya miundombinu ya vyoo shuleni hapo ili viweze kujengewa Kwa kukidhi mahitaji ya wenye ulemavu.
Katika ziara hiyo, wanawake wadau mbalimbali wakiongozwa na wanachama wa Tanga Woman Foundation walitoa msaada wa vyakula vya futari,sabuni,mavazi mbalimbali kwa ajili wanafunzi huku wazazi wao wakikabidhiwa vitenge.
"Kama tunavyowaona,wengine wanatembea Kwa kutambaa maana yake wanapoingia vyooni lazima washike kinyesi cha wenzao au uchafu mwingine maana yake hawa wanafunzi wapo katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya milipuko Kwa sababu miundombinu ya vyoo si rafiki"amesema Johnson
Afisa wanachama mwandamizi wa Mfuko wa Bima ya afya (NHIF) Mkoa wa Tanga,Macrina Clemens amesema wanawake hao wamejipanga kuwalipia gharama za kujiunga mfuko huo ili waweze kutibiwa wanapougua.
"Kwa kuwa wanawake hawa wameinesha njia baada ya kuguswa kuwalipia gharama za kuwaumganisha katika mfuko na sisi NHIF tutawalipia watoto wawili"amesema Macrina.
MWISHO
No comments:
Post a Comment